Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WANA KITU! Masupastaa hawa piga ua majina yao yatachomoza Ballon d’Or 2025

KITU Pict

Muktasari:

  • Supastaa huyo wa Real Madrid alishindwa kidogo tu kushinda tuzo hiyo mwaka jana, alipoangushwa na kiungo wa Manchester City, Rodri - uamuzi ambao ulizua sintofahamu kubwa katika kambi ya Mbrazili huyo wakilalamikia matokeo kwamba hayakuwa ya haki kwao.

LONDON, ENGLAND: VINICIUS Junior anakabiliwa na ushindani mkali kwenye vita ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or 2025.

Supastaa huyo wa Real Madrid alishindwa kidogo tu kushinda tuzo hiyo mwaka jana, alipoangushwa na kiungo wa Manchester City, Rodri - uamuzi ambao ulizua sintofahamu kubwa katika kambi ya Mbrazili huyo wakilalamikia matokeo kwamba hayakuwa ya haki kwao.

Ushindi wa Rodri uliwafanya Real Madrid kugomea sherehe hizo zilizofanyika Paris, Ufaransa baada ya mchezaji wao huyo kutoshinda.

Kiungo wa Kihispaniola, Rodri amepata maumivu ya goti yaliyomfanya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu msimu huu na hivyo hatakuwa na uwezo wa kutetea tuzo yake kwa mwaka 2025, jambo litakalotoa nafasi kwa washindani wengine kuchuana na Vini Jr kwenye kunasa tuzo ya Ballon d’Or.

Wachezaji wenzake Vini Jr kwenye kikosi cha Real Madrid, Kylian Mbappe na Jude Bellingham ni miongoni mwa wakali watakaochuana kuwania Ballon d’Or 2025, huku supastaa wa Liverpool, Mohamed Salah akitajwa kama mchezaji anayepewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi.

Msimu huu wa 2024/25 hauna michuano ya soka la kimataifa, hivyo mshindi atatazamwa kwa kiwango na mchango wake mkubwa aliofanya kwenye mechi za klabu.

Kutokana na hali ya mambo yalivyo hadi kufikia sasa msimu huu, hii hapa orodha ya mastaa 10 ambao panga pangua watapigana vibega kwenye kuwania tuzo hiyo ya Ballon d’Or 2025.


KT 10
KT 10

10. Virgil van Dijk, beki wa kati

Rekodi zake 2024/25: mabao 3, asisti 1

Kinachonogesha zaidi uwepo wa beki wa kati wa Liverpool kwenye kundi hilo ni kucheza mechi 20 bila ya timu yake kuruhusu bao. Ndiye nahodha wa Liverpool na amekuwa na kiwango bora msimu huu, akisaidia timu hiyo kuongoza msimamo wa Ligi Kuu England na Jumapili itacheza fainali ya Kombe la Ligi. Kwa hali ilivyo, Van Dijk, 33, atakwenda kushinda taji la Ligi Kuu England na kwenye tuzo za 2019, alishika namba mbili. Msimu huu, Liverpool yake imekomea hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na Jumapili itakipiga na Newcastle United uwanjani Wembley kwenye fainali ya Kombe la Ligi.


KT 09

9. Robert Lewandowski, straika

Rekodi zake 2024/25: mabao 34, asisti 3

Jina lililozoea kuwapo kwenye chati za juu za wafungaji mahiri kwenye ligi za Ulaya kwa zaidi ya muongo mmoja sasa. Na hakika, straika Robert Lewandowski haonekani kupunguza kasi yake ya kufunga mabao wakati sasa akitamba kwenye kikosi cha Barcelona chini ya kocha Hansi Flick. Kwenye La Liga amefunga mabao 21 msimu huu, huku akiwa kwenye umri wa miaka 36, anaendelea kuwa mchezaji muhimu katika kuisaidia timu yake kuchuana na timu za Real Madrid na Atletico Madrid kwenye mbio za ubingwa. Kiwango bora kinamweka Lewandowksi kwenye nafasi ya kushinda tuzo hiyo.


KT 08

8. Jude Bellingham, kiungo mshambuliaji

Rekodi zake 2024/25: mabao 11, asisti 11

Baada ya kushinda ubingwa wa La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita huko Real Madrid, ambapo ulikuwa msimu wake wa kwanza, kiungo mshambuliaji Jude Bellingham ameendelea kuonyesha kiwango bora kabisa kwenye kikosi hicho chini ya kocha Carlo Ancelotti. Mchango wake wa mabao pengine umepungua kwa kiasi fulani kwa msimu huu, lakini mchezaji huyo amekuwa muhimu kwelikweli katika kuisaidia Real Madrid, ambayo imeshatinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kwenye La Liga bado ipo kwenye vita kali ya kusaka ubingwa. Mwaka 2024, alishika namba tatu.


KT 07

7. Harry Kane, straika

Rekodi zake 2024/25: mabao 32, asisti 11

Baada ya miaka kibao ya kufunga mabao ya kutosha, straika Harry Kane yupo kwenye wakati mzuri wa walau msimu huu kubeba taji lake la kwanza katika maisha yake ya soka kutokana na Bayern Munich kujiweka kwenye nafasi kubwa ya kunyakua ubingwa wa Bundesliga. Bayern imejikita kileleni kwa tofauti ya pointi kibao dhidi ya mabingwa watetezi Bayer Leverkusen, huku Kane akiwa na mchango mkubwa katika kulifanya hilo, akiwa amefunga mabao 21 hadi sasa kwenye Bundesliga na kuwa kinara wa mabao. Kane amefunga mabao 10 pia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.


KT 06

6. Lamine Yamal, winga

Rekodi zake 2024/25: mabao 12, asisti 17

Umri wake ndio kwanza miaka 17, hivyo Lamine Yamal bado ana muda wa kuendelea kung’ara uwanjani kwenye mchezo wa soka kama anavyofanya kwa sasa, ambapo mwaka jana aliipa Hispania ubingwa wa Euro 2024 na msimu huu anatamba na Barcelona kwenye chati za juu katika La Liga. Kiwango chake bora kwenye Euro 2024 hakitahesabika kwenye Ballon d’Or 2025, lakini anachokifanya winga huyo akiwa na Barcelona msimu huu kinamweka kwenye wakati mzuri wa kuwamo kwenye tuzo hizo za Ballon d’Or. Kwenye ile fowadi ya Barcelona, Yamal anaongoza kwa asisti, 17.


KT 05

5. Ousmane Dembele, winga

Rekodi zake 2024/25: mabao 29, asisti 6

Akicheza kwa kiwango bora kabisa kwa muda mrefu, winga Mfaransa, Ousmane Dembele ameendelea kuwasha moto akiwa na kikosi cha Paris Saint-Germain msimu huu. Ndiye kinara wa mabao wa Ligue 1, akiwa amefunga mara 20 na kuiweka timu yake kwenye nafasi nzuri ya kushinda ubingwa wa Ufaransa kwa msimu huu. Lakini, kikubwa kinachompa nafasi syaa huyo kwenye mchakamchaka wa kushinda tuzo ya Ballon d’Or ni kiwango chake kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo amechangia mabao 10 na kuisaidia PSG kutinga kwenye hatua ya robo fainali ya mikikimikiki hiyo.


KT 03 (1)
KT 03 (1)

4. Vinicius Junior, winga

Rekodi zake 2024/24: mabao 18, asisti 11

Baada ya kuapa kwamba atahitaji kupiga hatua moja bora zaidi mwaka huu baada ya mwaka jana kushika namba mbili, Vinicius ameendelea kuonyesha kiwango bora sana kama ilivyokuwa 2023/24 akiwa chachu ya mafanikio kwenye kikosi chake cha Real Madrid. Licha ya kushika namba tano kwenye chati za kufunga mabao au kuasisti kwenye La Liga, winga huyo wa Kibrazili ameonyesha mchango mkubwa kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambako amefunga mabao saba katika mechi tisa huku akiifikisha timu yake katika hatua ya robo fainali. Macho yote kwa Vini tuzo za mwaka huu.


KT 03

3. Mohamed Salah, winga

Rekodi zake 2024/25: mabao 32, asisti 22

Kutokana na mkataba wake Liverpool kufika tamati mwishoni mwa msimu huu, wachache sana walikuwa na imani kwamba Mo Salah angekuwa na msaada mkubwa kwenye timu hiyo katika kupambania mataji msimu huu. Lakini, mkali huyo amekuwa moto kwelikweli akiwa na vijana hao wa Anfield, akiwa amefunga mara 27 kwenye Ligi Kuu England na kuasisti mara 17, hivyo kuwa kwenye mstari wa mbele kabisa katika mbio za kufukuzia Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya. Ubora wake wa uwanjani ulikuwa unamweka pazuri kwenye mbio za Ballon d’Or 2025 kabla ya Liverpool kutupwa nje.


KT 02

2. Raphinha, mshambuliaji

Rekodi zake 2024/25: mabao 27, asisti 19

Staa huyo wa zamani wa Leeds United, Raphinha ameshtusha wengi kutokana na kile anachokifanya kwenye kikosi cha Barcelona msimu huu. Amekuwa na kiwango bora sana kwenye safu ya washambuliaji watatu katika kikosi hicho cha kocha Flick, ambapo Raphinha amefunga jumla ya mabao 27 na kuasisti mara 19. Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambako Barcelona imetinga robo fainali, namba za Raphinha si mbaya, akifunga mabao 11 katika mechi 10. Hakuna Mbrazili mwingine aliyeshinda tuzo ya Ballon d’Or tangu Kaka alipofanya hivyo mwaka 2007, hivyo Raphinha anataka kuokoa jahazi.


KT 01

1. Kylian Mbappe, straika

Rekodi zake 2024/25: mabao 28, asisti 4

Baada ya kuanza kwa hasi hafifu kwenye kikosi cha Real Madrid, hatimaye Kylian Mbappe amejipata, ambapo sasa amekuwa mchezaji muhimu kwenye timu hiyo chini ya kocha Carlo Ancelotti. Akiwa amefunga mabao 18 kwenye La Liga, anazidiwa na Le- wando-wski tu kwenye kufunga mabao, huku mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2018, akiwa na mchango mkubwa kwenye timu yake kufanya vizuri kwenye La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa muda mrefu, Mbappe amekuwa akitamwa kama mrithi wa wakati wa soka, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo na anajaribu kupambana kufikia hilo.