Hii ndio jeuri ya Simba

YANGA ndio mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara baada ya kulitwaa kombe hilo mara 27 huku Simba ikilinyakua mara 20 na sasa wanalifukuzia mara ya 21.
Wakati Yanga ikitamba na rekodi hizo, Simba ndio timu yenye makombe mengi Tanzania tangu mwaka 1965 ikivuna jumla ya makombe 52.
Katika makombe hayo, Kombe la Ligi Kuu ndio imevuna mara nyingi (20) na ndio ilikuwa timu ya kwanza kubeba mwaka 1965 na 1966.
Simba ililibeba tena kombe hilo mwaka 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004 na 2007, msimu wa mwaka 2009/10. 2011/12, 2017/18 na msimu wa mwaka 2018/19
Pia Simba imenyakua Kombe la Nyerere ambalo sasa hivi halipo, walilolitwaa mara tatu mwaka 1984, 1985 na 2000, na mara ya mwisho kufanyika ilikuwa mwaka 2002 amabapo JKT Ruvu walilitwaa kombe mbele ya KMKM.
Kombe la Muungano imeshinda mara tano mwaka 1993, 1994, 1995, 2001, na 2002 na kombe la Mapinduzi ambalo Simba amelitwaa mara tatu mwaka 2008, 2011 na 2015.
Ubingwa wa Tusker umelibeba mara nne mwaka 2001, 2002, 2003 na 2005 na mara moja kombe la Banc ABE Super8 mwaka 2012 na Hedex mwaka 2001.
Mtani Jembe Simba ilichukua mara mbili mwaka 2012 na 2013 wakati kombe la FAT ikibeba mara tatu 1995,2000 na 2017.
Ngao ya Jamii imekwenda Msimbazi mara sita mwaka 2001, 2011, 2012, 2017, 2018 na 2019 huku Kagame nayo ikinyakua mara sita pia mwaka 1974, 1991, 1992, 1995, 1996 na 2002.
Rekodi nyingine tamu kwa simba imewahi kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1974, hatua ya makundi 2003 na robo fainali 2019 wakati fainali ilifika mwaka 1993.