Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaze atema wanne aleta wawili Yanga

KOCHA Cedric Kaze anataka kuona Yanga haishuki pale kileleni mwa msimamo hadi nwisho wa msimu, lakini anajua jambo hilo linahitaji juhudi za pamoja na kuwa na kikosi imara.

Katika kuifikia nchi ya ahadi, Kaze amefanya mabadiliko kadhaa kikosini ikiwamo kuwatoa kwa mkopo wachezaji wanne huku akiandaa wengine wawili kuingia kikosini.

Tayari Yanga imeshamtambulisha straika wake mpya Saidi Ntibazonkiza raia wa Burundi ambaye jana alianza kwa kishindo akipiga mbili safi na kuupiga mpira mwingi katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Singida United katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Liti ambao zamani ulifahamika kama Namfua.

Mwanaspoti linafahamu kwamba kocha wao Cedric Kaze amekabidhi ripoti kwa mabosi wake ya kuhitaji majembe wawili kwenye usajili wa dirisha dogo, straika na beki mzawa ambapo moja kwa moja jicho limetua kwa beki wa kushoto wa Namungo, Edward Charles Manyama aliyewahi kuichezea timu hiyo ya Jangwani miaka ya nyuma.

Kaze anavutiwa na beki huyo wa kushoto wa Namungo ambaye yupo katika wakati mzuri tangu msimu uliopita na juzi alifunga bao tamu la frii-kiki ya moja kwa moja mpaka katika sare ya 2-2 dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Azam Compkex.

Mbali na kukamilisha usajili wa Saido, Kaze pia anataka kumsajili straika wa kati, ambaye atamuweka wazi hivi karibuni wakihusishwa na Dark Kabangu kutoka DC Motema Pembe ya DRC.

Kaze anawatoa kwa mkopo Abdulaziz Makame kwenda Polisi Tanzania, Fahad Fuad (Coastal Union), Juma Mahadhi na Adam Kiondo ambao wanakwenda Ihefu kwa ajili ya kupata muda zaidi wa kucheza.

Kama Manyama atasajiliwa basi hii itakuwa ni mara ya pili kwa mchezaji huyo kwani aliwahi kuitumikia Yanga akitokea JKT Ruvu msimu wa 2014 na kudumu kwa misimu miwili tu kisha akatimkia zake Geita Gold.