Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ame apiga hesabu zake Simba

BEKI wa Simba, Ibrahim Ame amesema kitendo cha kuanza kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kinatoa taswira nzuri kwake katika kulinda kipaji chake.

Ame alisajiliwa Simba akitokea Coastal Union kabla ya kuanza kwa msimu huu lakini hakuwa akipata nafasi mbele ya Joash Onyango, Pascal Wawa, Kennedy Juma na Erasto Nyoni ambao wamekuwa wakichuana mara kwa mara.

Hivi karibuni beki huyu amepata nafasi ya kuanza na amekuwa akionyesha kiwango kizuri akicheza sambamba na Onyango.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ame alisema ni jambo zuri kwake kupata nafasi lakini ana kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba anaitumia vizuri fursa anayopata.

“Naona namba ninayo lakini sio rahisi sana kwani kuna wachezaji wengi eneo hili wana uwezo, kikubwa ambacho natakiwa kukifanya ni kuhakikisha kwamba sifanyi makosa ili kuendelea kuwa kwenye mipango ya kocha,” alisema beki huyo wa kati aliyesifika sana akiwa na Coastal ya Tanga.