Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lewandowsk kuikosa El Classico

LEWA Pict

Muktasari:

  • Lewandowski ambaye amekuwa katika kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu ambapo amefunga mabao 40 katika mechi 48 za michuano yote, aliumia katika mchezo wa wikiendi iliyopita dhidi ya Celta Vigo na Barcelona ililazimika kurudi ikitokea nyuma kwa mabao.

BARCELONA, HISPANIA: STRAIKA wa Barcelona, Robert Lewandowski anatarajiwa kuukosa mchezo wa El Classico dhidi ya Real Madrid baada ya kupata majeraha ambayo yatamweka nje kwa Zaidi ya wiki tatu.

Lewandowski ambaye amekuwa katika kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu ambapo amefunga mabao 40 katika mechi 48 za michuano yote, aliumia katika mchezo wa wikiendi iliyopita dhidi ya Celta Vigo na Barcelona ililazimika kurudi ikitokea nyuma kwa mabao.

Lewandowski alionekana akitoka uwanjani baada ya kuumia misuli ya paja.

Ripoti za awali zilieleza kulikuwa na hali ya wasiwasi ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo kuhusu jeraha la nyota huyo mwenye umri wa miaka 36, huku timu ikihofia kuwa ameumia misuli jambao lililothibitika kweli, baada ya kumfanyia vipimo Zaidi.

Makadirio Ukubwa wa jeraha hilo na muda wa kupona inadaiwa inaweza kuchukua wiki tatu au zaidi itategemea na namna mwili wake utakavyokuwa.

Katika kipindi ambacho Barcelona itakuwa inamkosa nyota huyu, itakuwa na mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Inter Milan (mchezo wa mkondo kwanza), pamoja na fainali ya Copa del Rey dhidi ya mahasimu wao wakubwa Real Madrid wikiendi ijayo.

Pia atakosa mechi za La Liga dhidi ya Mallorca na Valladolid. vilevile, huenda akakosa michezo mingine kama ule wa marudiano dhidi ya Inter Milan na pambano muhimu la ligi dhidi ya Real Madrid.

Jambo zuri kwa Flick ni Dani Olmo amerudi na Ferran Torres pia anaweza akatumika kwenye eneo hilo kutokana na kiwango bora ambacho anacho kwa sasa, hata hi yuko kwenye kiwango kizuri kwa Barcelona. Hata hivyo, ushirikiano wa Lewandowski na Raphinha pamoja na Lamine Yamal ulikuwa ni wa muda mrefu na ulishazoeleka.