Arsenal waibeba Man United England

Muktasari:
- Iko hivi, Man United ambayo kwa sasa ina pointi 38, ikiwa imeshacheza mechi 33, bado ilikuwa katika hatari ya kushuka daraja kwani pointi hizo zilikuwa zinaweza kufikiwa na Ipswich Town inayoshika nafasi ya 18.
LONDON, ENGLAND: BAADA ya kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ipswich Town, Arsenal imeiondolea presha Manchester United juu ya suala la kushuka daraja.
Iko hivi, Man United ambayo kwa sasa ina pointi 38, ikiwa imeshacheza mechi 33, bado ilikuwa katika hatari ya kushuka daraja kwani pointi hizo zilikuwa zinaweza kufikiwa na Ipswich Town inayoshika nafasi ya 18.
Hata hivyo, baada ya Ipswich yenye pointi 21, kupoteza dhidi ya Arsenal haitoweza kufikia pointi za Man United hata ikishinda mechi zake tano zilizosalia.
Kwa sasa katika mechi hizo tano, Ipswich hata ikishinda zote itafikisha pointi 36 tu wakati kama ingepata ushindi dhidi ya Arsenal kisha ikashinda mechi zake tano jumla ingekuwa na pointi 39.
Mbali ya mchezo huu uliopigwa jana, pia kulikuwa na michezo mingine ambayo ni Fulham dhidi ya Chelsea uliomalizika kwa Chelsea kushinda mabao 2-1.
Vilevile Manchester United nayo iliambulia kichapo cha bao 1-0 kutoka Wolves ambao ushindi huo uliwawezesha kufikisha pointi 38 na kujisogeza katika nafasi ya 15.