Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United, Osimhen ni suala la muda

MAN UTD Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa nyota huyo tayari amesaini makubaliano ya kujiunga na Man United dirisha la usajili la majira ya kiangazi na inaweza kumpata kwa Pauni 25 milioni tu.

MANCHESTER, ENGLAND: IMEFICHUKA. Ripoti zinadai kuna uwezekano mkubwa straika wa Napoli anayecheza kwa mkopo Galatasaray, Victor Osimhen akacheza Manchester United msimu ujao baada ya kukubaliana na miamba hiyo ya Old Trafford.

Inaelezwa nyota huyo tayari amesaini makubaliano ya kujiunga na Man United dirisha la usajili la majira ya kiangazi na inaweza kumpata kwa Pauni 25 milioni tu.

Mmoja wa watu wa karibu wa Osimhen amefichua tayari kuna makubaliano binafsi kati ya mchezaji huyo na Manchester United, ingawa bado hakuna makubaliano kati ya Man United na  Napoli.

Nyota huyo wa kimataifa wa Nigeria anatarajiwa kurejea Napoli mara baada ya msimu huu kumalizika, baada ya kutumia msimu huu kwa mkopo na Galatasaray.

Mwandishi wa habari wa Uturuki, Serdar Ali Celikler kupitia NEO Spor alifichua Osimhen ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026 ameshafikia hadi makubaliano ya mshahara.

Inaelezwa Napoli inapambana kumuuza dirisha lijalo kwa sababu ya muda uliobaki katika mkataba wake wakiamini ikiwa itashindikana kumuuza mwisho wa msimu huu, wanaweza kumuuza kwa kiasi kidogo cha pesa.

Taarifa kutoka tovuti ya Africa Foot imeongeza, watu wa karibu wa staa huyo 'wanafurahia sana' wazo la fundi huyu kuhamia Ligi Kuu England.

Man United wamekuwa wakimfuatilia Osimhen kwa muda mrefu na matatizo yao ya kufunga mabao chini ya kocha Ruben Amorim yamezidisha juhudi za kumsajii.

Kulikuwa na mazungumzo ya mabadilishano ya wachezaji kati ya Napoli na United  Januari mwaka huu na Napoli walikuwa wanahitaji Saini ya Alejandro Garnacho baada ya fundi huyo kutoka Argentina kuweka nje mechi kadhaa na Amorim ambaye alidai haridhishwi na utendaji kazi wake.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Osimhen amefunga mabao 29 katika mechi 34 msimu huu, yakiwemo mabao 21 ya  Ligi Kuu  Uturuki (Super Lig).

Osimhen alijiunga na Galatasaray dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana baada ya Napoli kumsajili Romelu Lukaku na kumpa nafasi ya kuondoka kama alivyohitaji.

Wawakilishi wake walifanya mazungumzo Chelsea, Paris Saint-Germain na baadhi ya timu za Saudi  Arabia, lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa hali iliyosababisha atue Galatasaray kwani hata dirisha la usajili katika ligi tano bora barani Ulaya lilishafungwa.