Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Martinelli amekataliwa mara nne Man United

Muktasari:

Kocha, Unai Emery aliona kipaji cha mchezaji huyo na kuamua kwenda kumsajili kwa Pauni 6 milioni kutokea klabu ya Ituano ya Brazil kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

LONDON, ENGLAND.STRAIKA, kinda anayeibukia kwa kasi huko Arsenal, Gabriel Martinelli ameripotiwa kufanya majaribio mara nne kwenye kikosi cha Manchester United na kupigwa chini mara zote hizo.
Lakini, sasa akiwa ndani ya uzi wa Washika Bunduki wa London, Martinelli amekuwa moto balaa, akifunga mara mbili kwenye mchezo wa Europa League wakati timu hiyo ilipoichapa Standard Liege 4-0.
Jambo hilo limemfanya Martinelli kufunga mabao manne katika mechi mbili baada ya kutupia mara mbili pia kwenye mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Nottingham Forest.
Kocha, Unai Emery aliona kipaji cha mchezaji huyo na kuamua kwenda kumsajili kwa Pauni 6 milioni kutokea klabu ya Ituano ya Brazil kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Lakini, kwa sasa mambo yangekuwa tofauti kwamba fowadi huyo angekuwa kwenye kikosi cha Man United akitamba na makinda wengine kama Mason Greenwood kama asingekataliwa mara nne wakati alipokwenda kufanya majaribio huko Carrington.