Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muguna: Nimekuja kufanya kazi

AZAM FC wanasajili tena. Wanasajili kweli kweli, ikiwa na maana kwamba wachezaji wanaowasajili ni wa viwango vya juu.

Timu hiyo inajiandaa na mashindano mbalimbali ya msimu ujao ikiwemo Ligi Kuu Bara na michuano ya Kimataifa kwani wamepata nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika.

Usajili unaoendelea kufanywa na viongozi wa Azam kwa kufuata ripoti ya Benchi la Ufundi ni dhahiri kwamba unaenda kuua ufalme wa wazawa hasa safu ya kiungo baada ya kusajili nyota wa kigeni wawili nafasi hiyo.

Azam imemalizana na kiungo, Paul Katema na Kenneth Muguna nyota hao wanaongeza changamoto kwa wazawa ambao miaka mingi wamekuwa wakishindanishwa wao kwa wao ambao ni, Frank Domayo, Mudathil Yahya na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Ujio wa nyota hao wa kimataifa utaongeza ushindani wa namba kikosini na kuwaongeza chachu ya upambanaji wazawa ili waweze kuendeleza heshima waliyoijenga ndani ya timu hiyo.

Mwanaspoti limefanya mahojiano maalumu na Muguna ambaye ni raia wa Kenya aliyefunguka mengi kuhusu soka la Tanzania na namna alivyojipanga kuhakikisha anaisaidia timu hiyo kufikia mafanikio.


AZAM KITAMBO TU

Siku moja baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia Azam aliliambia Mwanaspoti kuwa tangu msimu uliopita matajiri wa jiji la Dar es Salaam walionyesha nia ya kutaka kumsajili lakini kutokana na mkataba wake kumfunga alishindwa kufanya hivyo.

“Nimejiunga na timu hii kutokana na kuvutiwa na namna ya uendeshwaji wake wa kisasa na pia ina kila sifa za kuitwa chuo cha uendeshaji soka kutokana na kuwa na kila kitu kinachotakiwa kwa mwanamichezo,” anasema


AMTAJA FEI TOTO

Kiungo huyo anasema anawafahamu wachezaji wengi wa Tanzania na amefanikiwa kucheza nao baadhi akiwa timu yake ya taifa huku akimtaja kiungo wa Yanga Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuwa ni miongoni mwa wachezaji anaowafahamu.

“Nawafahamu wengi tangu nimecheza nao kwenye mashindano mbalimbali nikiwa timu ya taifa sitaki kuzungumza mengi kuhusu wao ila nawaheshimu ni wachezaji wazuri mmoja wao ni Fei Toto kama sijakosea,” anasema.


AMKANA KIONGERA

Ujio wa Muguna kwenye soka la Tanzania kutoka Kenya sio wa kwanza kutokea kwani alishawahi kutua mshambuliaji.

Paul Kiongera, Danny Serunkuma walishindwa kumudu soka la Bongo kama wengi walivyotarajia kutokana na namna ambavyo walionyesha viwango vya juu kwenye ligi yao ya Kenya.

“Nimekuja kama Muguna na sio Kiongera wala hao wengine sitaki kufananishwa na waliopita naomba kupimwa kwa uwezo nitakaouonyesha sijaja kuzungumza sana nimekuja kufanya kazi muda utazungumza,” anasema Muguna.


KIRAKA

Kiungo huyo ameendelea kuielezea Mwanaspoti yeye ni kiraka.

“Nimezaliwa kwaajili ya kucheza mpira sioni kama kuna kitu ningekua nafanya tofauti na mpira, hivyo kuhusu nafasi ya kucheza nitacheza mahali popote kocha atakaponipanga isipokuwa kipa kikubwa ni kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri,” anasema.


HAOFII CHOCHOTE

“Sina wasiwasi na Ligi ya Tanzania najua viongozi wangu wanachokitarajia kutoka kwangu hivyo kutokana na uzoefu nilionao nitapambana kwa hari na mali ili nihakikishe nafanya zaidi ya yale wanatoyatarajia.

“Nafahamu sio kazi rahisi kwangu kutokana na ugeni wangu ndani ya nchi hii pamoja na ligi kikubwa ninachoomba ni ushirikiano kutoka kwa wenyeji wangu ili kuweza kufikia mafanikio,” anasema.