Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF: Hakuna ruksa mchezaji kuondoka

WACHEZAJI wengi mikataba yao inaelekea ukingoni na wengine kumalizika mwezi huu, huku wasijue nini cha kufanya wakati muda wowote ligi ikitarajia kuendelea.

Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Wanachama kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Rahim Shabany alisema wachezaji watabaki kuwa mali ya timu hadi ligi inapoisha.

“Kisheria kama ligi inaendelea lazima wamalizie msimu na baada ya hapo watakuwa huru kama mchezaji kuna timu anahitaji kwenda atafanya hivyo mwishoni.

“Tuchukulie kuna mchezaji anayechezea Mtibwa halafu kutokana na hii hali akasajiliwa na Lipuli na tunakwenda kumalizia mechi za msimu huu hapo utaona kuna mkanganyiko, hivyo lazima amalize msimu na timu yake ya sasa,” alisema Shabany.

Aliongeza wachezaji wote ambao mikataba yao imemalizika na inamalizika kabla ya ligi kuisha wanapaswa kumalizia kwanza michezo iliyobaki ndipo taratibu nyingine ziendelee.

Aliwakumbusha viongozi wa timu pamoja na wachezaji kuzingatia sheria na kanuni ya muda gani mchezaji anapaswa kufanya mazungumzo na timu nyingine.

Hivi karibuni Fifa ilitaka wachezaji wanaomaliza mikataba yao kusubiri hadi pale ligi za nchi zao zitakapomalizika baada ya kuahirishwa kutokana na janga la corona linalotikisa dunia.

Mbali na wachezaji wanaomaliza mikataba, lakini pia klabu zinazoingia mikataba na wachezaji wapya nchini kipindi hiki zitatakiwa kufuata maelekezo ya Fifa na Caf kama yalivyoelekezwa.

“Muda wa usajili bado, utaratibu wa awali umevurugika na Caf na Fifa wametoa muongozo mpya wa lini muda mzuri wa kuanza usajili na zoezi lifungwe lini,” alisema mmoja wa viongozi wa juu wa TFF ambaye hakutaka kuandikwa jina.

Kutokana na janga hilo, Fifa ilitaka wachezaji ambao mikataba yao inaelekea ukingoni kusubiri hadi pale ligi za nchi zao zitakalomalizika.

Baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao inaelekea ukingoni ni Bigirimana Blaise, Reliants Lusajo (Namungo FC), Darueshi Saliboko (Lipuli FC), na Sixtus Sabilo (Polisi Tanzania).