Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ahly, Wydad zimevuna zilichopanda Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Kilichotusikitisha zaidi hapa kijiweni ni Wydad Casablanca na Al Ahly kuaga mashindano hayo bila kupata ushindi angalau katika mechi moja jambo ambalo wengi hatukulitegemea kabla mashindano hayo hayajaanza.

MAMBO yameonekana kuwa magumu sana kwa wawakilishi wa Afrika katika Fainali za Kombe la Dunia la Klabu zinazoendelea huko Marekani.

Kilichotusikitisha zaidi hapa kijiweni ni Wydad Casablanca na Al Ahly kuaga mashindano hayo bila kupata ushindi angalau katika mechi moja jambo ambalo wengi hatukulitegemea kabla mashindano hayo hayajaanza.

Ilipaswa hata kama hazikuwa vizuri basi angalau zingejitahidi kutafuta vibonde wao na kujipigia na sio kutolewa huku ushindi zikiwa zimeusikia katika bomba kwani hiyo inatoa maana kuwa hizo timu ni dhaifu na hauwezi kumbishia anayeamini hivyo.

Hata hivyo, hapa kijiweni tumechagua kutozilaumu Al Ahly na Wydad Casablanca kwa vile kilichotokea kwa hizo timu kilipaswa kitokee na ingekuwa jambo la kushangaza zaidi iwapo matokeo ambayo zilipata yasingetokea na zingefanya vizuri.

Ukianzia kwa Al Ahly, sayansi ya soka ilikuwa inapingana na wao kutamba kwenye mashindano hayo kwa vile walifanya maboresho ya benchi lao la ufundi, wiki mbili kabla ya Fainali za Kombe la Dunia la Klabu kuanza ambapo Kocha Jose Riveiro alianza rasmi kuinoa timu hiyo akichukua mikoba iliyoachwa na Marcel Kohler.

Katika hali ya kawaida hakuna kocha anayeweza kuifanya timu kuwa tishio huku akiwa ameifundisha kwa muda wa wiki mbili tu. Labda maajabu tu yatokee lakini kiuhalisia ni nadra sana.

Na kwa bahati mbaya kwa Riveiro ni kwamba alijiunga na timu ambayo hali ya kisaikolojia haikuwa nzuri kwa vile imetoka kuyakosa mataji muhimu na makubwa ambayo ilipanga kuyatwaa msimu huu.

Wydad yenyewe haikuwa na msimu mzuri na hilo likapelekea ifanye usajili wa nyota zaidi ya wanne katika dirisha hili la usajili ili angalau wawe na baadhi ya nyota ambao wataifanya iwe na ushiriki mzuri kwenye hayo mashindano lakini mwishowe ni vigumu kwa wachezaji kuzoeana ndani ya muda mfupi.

Hata hivyo, watajijua wenyewe, sisi furaha yetu ni kuona mtoto wa Tanzania, Selemani Mwalimu 'Gomez' akipta dakika za kutosha za kucheza tena katika mechi dhidi ya timu kubwa kama Juventus.