Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgaza miwili tena Dodoma Jiji

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo alijiunga na Dodoma jiji Julai 2023 akitokea KMKM ya Zanzibar, ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili ambao umefikia ukingoni msimu huu. Umuhimu wake kikosini hapo umempa ulaji mpya.

MABOSI wa Dodoma Jiji, wamemalizana na mshambuliaji wao, Yassin Mgaza kwa kumuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi msimu wa 2026-2027.

Mshambuliaji huyo alijiunga na Dodoma jiji Julai 2023 akitokea KMKM ya Zanzibar, ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili ambao umefikia ukingoni msimu huu. Umuhimu wake kikosini hapo umempa ulaji mpya.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Dodoma Jiji, kimeliambia Mwanaspoti mshambuliaji huyo bado ni mali ya timu hiyo kwa misimu mingine miwili licha ya kutoonyesha ubora kutokana na majeraha ya mara kwa mara.

“Ni kweli hakuwa vizuri msimu uliomalizika lakini kocha amekiri ni mchezaji mzuri, anahitaji muda zaidi ili kufanya kazi nzuri ndani ya timu, makubaliano tuliyofikiana naye tunatarajia mambo mazuri msimu ujao,” alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza.

“Hatujawa bora sana kama timu msimu uliomalizika lakini malengo tumeyafikia kwa sababu tumebaki kucheza msimu ujao, mipango muhimu inatakiwa kufanyika mapema mwaka huu ili msimu ujao tufikia malengo kwa kumaliza nafasi tano za juu.”

Alisema hawawezi kuanza usajili wa nje moja kwa moja kabla hawajabakiza wakezaji muhimu ambao wanaamini wataendelea kupambania nao mafanikio.

Dodoma Jiji imemaliza msimu huu ikiwa nafasi ya 12 baada ya kucheza mechi 30, imeshinda tisa, sare saba na vipigo 14 ikifunga mabao 31 na kuruhusu nyavu zake kutikishwa mara 49.