Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam yasaka rekodi Kombe la Muungano

Muktasari:

  • Azam ni miongoni mwa timu zinazoshiriki michuano hiyo mwaka huu itakayoanza kutimua vumbi kuanzia Aprili 23 hadi 30, visiwani Zanzibar, huku rekodi zikionyesha ni klabu mbili pekee kati ya nane zinazoshiriki zilizowahi kutwaa taji hilo.

BAADA ya ndoto za Azam kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kuota mbawa, kocha Rachid Taoussi kwa sasa amehamishia nguvu katika michuano ya Kombe la Muungano, ingawa anakabiliwa na mtihani mkubwa wa kuchukua taji hilo.

Azam ni miongoni mwa timu zinazoshiriki michuano hiyo mwaka huu itakayoanza kutimua vumbi kuanzia Aprili 23 hadi 30, visiwani Zanzibar, huku rekodi zikionyesha ni klabu mbili pekee kati ya nane zinazoshiriki zilizowahi kutwaa taji hilo.

Timu zilizowahi kuchukua ubingwa wa michuano hiyo, ni Yanga iliyochukua mara sita sawa na wapinzani wao wa jadi, Simba ambayo haitashiriki kutokana na ratiba ya Kombe la Shirikisho Afrika kubana na nafasi yake kuchukuliwa na Singida Black Stars.  Nyingine iliyowahi kutwaa taji hilo ni KMKM iliyochukua mara moja mwaka 1984, hivyo sita zilizobakia ambazo ni Azam FC, Coastal Union, Singida Black Stars, JKU, KVZ SC na Zimamoto FC zinashiriki zikisaka rekodi mpya ya kuchukua ubingwa huo.

Akizungumzia suala hilo, Taoussi alisema licha ya ugumu wa michuano hiyo ila atahakikisha wanaitumia vyema kuweka rekodi mpya ya kuchukua taji hilo kwa mara ya kwanza, ili wamalize angalau kwa heshima baada ya kufanya vibaya katika Ligi Kuu.

“Hii ni nafasi nyingine kwetu ya kufanya vizuri na kumaliza na taji lolote msimu huu, ni michuano mizuri ila ni migumu kwa sababu inachezwa kwa njia ya mtoano, hivyo inahitaji nidhamu ya hali ya juu ili kutimiza malengo,” alisema Taoussi.

Azam FC itaanza kuisaka tiketi ya kufikia nchi ya ahadi kwa kucheza na KMKM FC, Aprili 24 na ikishinda itaenda hatua ya nusu fainali, ambapo itacheza na mshindi kati ya JKU SC au Singida Black Stars zitakazofungua michuano hiyo, Aprili 23.

Michuano hii inafanyika mwaka wa pili mfululizo kufuatia kufanyika pia 2024, baada ya kutofanyika kwa kipindi cha miaka 22, tangu mara ya mwisho ilipofanyika 2002, huku Simba ikiwa ndio bingwa mtetezi wa taji hilo ilipolichukua mwaka jana.