Beki Yanga Princess bado anajifunza

Muktasari:
- Tangu amesajiliwa Yanga amekuwa akipata nafasi chache za kucheza tangu kocha Mzambia, Charles Haalubono na sasa Edna Lema ‘Mourinho’.
LICHA ya kutopata nafasi kwenye kikosi cha Yanga Princess, lakini beki wa kulia, Lucy Pajero amesema anajifunza vitu vingi akiwa benchi.
Beki huyo alisajiliwa msimu 2022/23 akitokea The Tigers Queens iliyoshuka daraja msimu huo.
Tangu amesajiliwa Yanga amekuwa akipata nafasi chache za kucheza tangu kocha Mzambia, Charles Haalubono na sasa Edna Lema ‘Mourinho’.
Akizungumza na Mwanaspoti, Pajero alisema akiwa benchi au hata jukwaani anajifunza vitu vingi kwenye karia yake ambavyo vinaweza kumsaidia.
“Hakuna sehemu utafanya kazi bila changamoto, na hilo litakupa nafasi ya kufikiria kipi unapaswa kukiongeza na mimi huwa nawafuatilia wenzangu wanachofanya ili niwe bora,” alisema Pajero.
Nafasi anayocheza beki huyo wapo nyota kama Protasia Mbunda aliyeingia kikosini hapo dirisha dogo na kuanza vizuri, Diana Mnally, Silvia Mwacha na Wema Maile.