Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama la Wana laing'oa Fountain Gate FA

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Dakika 90 za pambano hilo liliisha kwa sare ya bao 1-1, kabla ya penalti kuitupa nje Fountain ikiungana na Dodoma Jiji, Tanzania Prisons na Azam FC zilizoaga katika hatua tofauti na kuiacha Stand iliyopo Ligi ya Championship ikisonga mbele hatua ya 16 Bora.

FOUNTAIN Gate imekuwa timu ya nne ya Ligi Kuu Bara kung'olewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho (FA), baada ya jioni hii kufungwa kwa penalti 4-3 na Stand United 'Chama la Wana' licha ya kucheza kwenye uwanja wa nyumbani wa Tanzanite Kwaraa, uliopo mjini Babati, Manyara.

Dakika 90 za pambano hilo liliisha kwa sare ya bao 1-1, kabla ya penalti kuitupa nje Fountain ikiungana na Dodoma Jiji, Tanzania Prisons na Azam FC zilizoaga katika hatua tofauti na kuiacha Stand iliyopo Ligi ya Championship ikisonga mbele hatua ya 16 Bora.

Dodoma ilitolewa mapema hatua ya 64 na Leo Tena, huku Prisons na Azam ziking'olewa na timu za Bigman na Mbeya City zilizopo Ligi ya Championship kama ilivyokuwa kwa Fountain katika hatua ya 32 Bora.

Katika mchezo wa leo Fountain inayonolewa na kocha Mkenya, Robert Matano ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 40 likifungwa na nyota wao Elia Mukono kabla ya Chama la Wana kuchomoa dakika ya 70 kupitia kwa mtokea benchi Msenda Msenda aliyekwamisha bao tamu.

Licha ya timu zote kuongeza kazi ya mashambulizi kutokana na mabadiliko kadhaa ya wachezaji katika kipindi hicho cha pili mambo yalibaki kama yalivyo kwa ubao kusomeka sare ya 1-1 ndipo zikafuta penalti na Chama la Wana ikakwamisha nne dhidi ya tatu za wenyeji.

Kwa matokeo hayo, Stand United sasa itavaana na Girrafe Academy katika mechi ya 16 Bora zinazoanzwa kupigwa kuanzia Alhamisi hii ili kusaka tiketi ya robo fainali ikiwa ni safari ya kusaka ubingwa wa michuano hiyo unaoshikiliwa na Yanga kwa misimu mitatu mfululizo sasa.

Bingwa wa michuano hiyo ndio anayeiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo kwa msimu huu Simba imefanikiwa kutinga robo fainali na inajiandaa kuvaana na Al Masry ya Misri mechi ya mkondo wa kwanza itakayopigwa ugenini Aprili 1-2.


Timu zilizotinga 16 na mechi zao zitakavyokuwa ni kama ifuatavyo;

Mbeya City v Mtibwa Sugar

Tabora Utd  v Kagera/Namungo

Mashujaa  v Pamba Jiji/Kiluvya

Stand United   v Gerrafe Academy

Yanga/Coastal   v Songea United

Singida BS  v KMC

JKT Tanzania  v Mbeya Kwanza

Simba/TMA  v BigMan