Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diao anateseka kwa Bacca, Job

Muktasari:

  • Raia huyo wa Senegal (22), ambaye ameichezea Azam misimu miwili mfululizo ameweka rekodi ya kufunga mabao matatu muda wote alioitumikia klabu hiyo amesema wachezaji hao ndio waliompa shida katika kukabiliana nao kwenye uwanja wa mechi.

MSHAMBULIAJI wa Azam, Alassane Diao amesema tangu aanze kucheza Ligi Kuu Bara nyota waliompa wakati mgumu ni Ibrahim Bacca na Dickson Job.

Raia huyo wa Senegal (22), ambaye ameichezea Azam misimu miwili mfululizo ameweka rekodi ya kufunga mabao matatu muda wote alioitumikia klabu hiyo amesema wachezaji hao ndio waliompa shida katika kukabiliana nao kwenye uwanja wa mechi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Diao alisema muda wote ambao amecheza Bara amekutana na safu ngumu zaidi ya ulinzi ya Yanga kuliko timu nyingine.

Kikosi cha Yanga chini ya mabeki hao kimeruhusu mabao 10 katika Ligi Kuu Bara msimu huu ikiwa miongoni mwa safu zilizoruhusu machache zaidi kikifuatiwa na Simba iliyoruhusu 13.

Alisema kuwa hadi sasa bado hajaona walinzi ambao wana uwezo na uzoefu wa kucheza muda mrefu kama mastaa hao wawili ambao wanaunda pacha hatari katika ligi hiyo. “Safu ya ulinzi Yanga ndio yenye wachezaji wagumu zaidi, lakini pia waliocheza pamoja kwa muda mrefu, hivyo wana muunganiko mzuri. Job na Bacca wana faida kubwa mbili kwanza wanazungumza lugha moja na pia wamecheza muda mrefu,” alisema.

“Kwa upande wa Azam ni David Fuentes Mendoza ambaye amekuwa akinipa wakati mgumu hasa mazoezini kutokana na ubora wake.”

Diao ambaye hajapata nafasi ya kucheza muda mwingi msimu huu kutokana na majeraha alirejea ndani ya kikosi hicho baada ya dirisha dogo la Januari, mwaka huu.

Mwanaspoti liliwahi kuripoti kuwa miongoni mwa mastaa ambao Azam itaachana nao msimu huu ni pamoja na mshambuliaji huyo. Azam katika msimamo wa Ligi Kuu Bara iliyomalizika hivi karibuni inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 63, ikicheza mechi 30, kushinda 19, sare sita na kupoteza tano.