Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fei Toto aipa pigo Azam FC

FEI Pict

Muktasari:

  • Katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa Azam Complex wenyeji walishinda bao 1-0, Fei Toto ndiye aliyekwamisha mpira wavuni kwa mkwaju wa penalti.

KIKOSI cha Azam kipo Bukoba kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, lakini kikiwa na pigo baada ya kiungo mshambuliaji nyota, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kutokuwepo kutokana na kuwa majeruhi, huku kocha akidai kuvurugwa kwa kumkosa.

Inaelezwa nyota huyo anayeongoza kwa asisti katika ligi akiwa nazo 13 ameshindwa kuambatana na timu kwa sababu ya kuwa na maumivu ya mguu, jambo lililomfanya kocha Rachid Taoussi kujipanga upya jeshi aliloenda nalo ugenini ili kukamilisha lengo la kuondoka na pointi tatu muhimu Azam inavaana na Kagera Sugar, huku kila moja ikiwa imecheza mechi 26 na hadi sasa Wanalambalamba wakishika nafasi ya tatu na pointi 51, wakati wenyeji wao wakiwa nazo 22 wakikamata nafasi ya 15, hali inayoufanya mchezo huo kuwa mgumu kwa kila moja ikihitaji pointi ili kujiweka pazuri zaidi ya ilipo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Taoussi alisema ni kweli wamemuacha Fei jijini Dar es Salaam ili aendelee na matibabu akitarajia kumtumia kwa mechi zilizosalia kabla ya kufunga msimu Mei 25.

“Fei amepata maumivu ya mguu, ila naamini atakuwa sawa hadi pale tutakaporejea ili aweze kujiandaa na mechi muhimu zijazo, zikiwamo za michuano ya Kombe la Muungano na zile za Ligi Kuu,” alisema Taoussi.

Azam ina kikosi kipana licha ya kuwa na pengo la nyota huyo litaonekana ila matumaini yao ni kutoka na alama tatu ugenini.

Katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa Azam Complex wenyeji walishinda bao 1-0, Fei Toto ndiye aliyekwamisha mpira wavuni kwa mkwaju wa penalti.

F 02

MECHI YENYEWE

Mechi ya Kagera na Azam ni kati ya michezo miwili inayopigwa leo Jumamosi, nyingine ikiwa ni kati ya Singida itakayoialika Tabora United kwenye Uwanja wa Liti, Singida huku wageni wakiwa ametoka kupoteza mechi nne mfululizo.

Tuanze na mechi ya Kaitaba. Kagera iliyopo chini ya Juma Kaseja inapambana kuepuka kushuka daraja na leo itakuwa na kazi ya kujinusuru baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo za ugenini dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji.

Kaseja aliyekabidhiwa timu  karibuni alianza vyema kwa kuiongoza Kagera kushinda mechi mbili mfululizo za ligi na moja ya Kombe la Shirikisho kabla ya mambo kumbadilikia na leo atakuwa na kibarua kigumu mbele ya Azam inayowania kumaliza ndani ya tatu bora ili ikate tiketi ya CAF.

Kibarua zaidi kinatokana na ukweli wageni wao nao wametoka kupoteza mechi mbili mfululizo mbele ya Yanga na Singida Black Stars, jambo ambalo linaisukuma kila timu kutaka kuondoka na pointi tatu ili kujiweka salama, huku wenyeji wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa duru la kwanza ugenini.

Peter Lwasa ndiye aliyeshika tumaini la eneo la ushambuliaji la Kagera akiwa na mabao manane, huku  nyota wengine kama Nassor Kapama, Abdallah Mfuko, Moubarack Amza na wakiwa na kazi kuisaidia timu kusahihisha makosa nyumbani. Azam upande wake itamtegemea Nassoro Saadun, Gibril Sillah na Zidane Sereri kufumania nyavu, huku nyota wengine akiwamo kipa Zubeiry Foba wakiwa na kazi ya kuinusuru isipoteze mchezo wa tatu. Makocha wa timu hizo wametambiana kila mmoja akisema dakika 90 za mchezo utakaopigwa kuanzia saa 1:00 usiku ndizo zitakazoamua.

F 04

SINGIDA BS v TABORA UTD

Singida iliyotoka kutibuliwa na Coastal Union katika mechi iliyopita baada ya awali kuizima Azam itakuwa nyumbani kuikaribisha Tabora United katika mchezo mwingine mkali wa ligi, huku timu hizo zikifukuzana katika msimamo Singida ikiwa ya nne na Nyuki wa Tabora wakiwa wa tano. Hilo ni pambano la nne kwa timu hizo kukutana katika Ligi Kuu Bara tangu Tabora ipande daraja msimu uliopita, huku rekodi zikiibeba zaidi Singida kwani imeshinda moja na michezo miwili imeisha kwa sare tofauti.

Wenyeji wanazitaka pointi tatu wakiiombea mabaya Azam mbele ya Kagera usiku kwani ikipata matokeo itawateremsha matajiri wa Jiji la Dar es Salaam kwa pointi mbili. Hata hivyo, Tabora United itakuwa na kibarua cha kupambania pointi tatu muhimu baada ya kutoka kupoteza mechi tano mfululizo, ikiwamo ya Kombe la Shirikisho ikianza na kichapo cha 2-1 mbele ya  JKT Tanzania kulazwa 2-1 na Kagera Sugar, wakatandikwa 3-1 na Yanga kisha kulala 1-0 katika Shirikisho dhidi ya Pamba Jiji na kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Mashujaa. Kwa upande wa Singida katika mechi  tano imefungwa mara moja na Coastal Union mabao 2-1 huku ikishinda mechi nne dhidi ya Kagera Sugar 2-0, Azam FC 1-0, Fountain Gate 3-0 na KMC 1-0.

F 03

Wenyeji Black Stars wanamtegemea Jonathan Sowah ambaye ameingia dirisha dogo na kuonyesha makali akiingia kambani mara tisa kati ya mechi tisa alizocheza, Elvis Rupia mwenye mabao 10 na nyota wengine.

Wakati Tabora wakiwa na kinara wa mabao kwenye kikosi Offen Chikola ambaye amepachika saba kambani na Heritier Makambo aliyetupia mabao matano.


F 01

NAMUNGO v MASHUJAA

Mechi hiyo itapigwa kesho Jumapili kuanza saa 1:00 usiku kwa wenyeji Namungo kuikabirisha Mashujaa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi kila moja ikipiga hesabu za kujiokoa eneo ilipo na kujiweka pazuri.

Namungo iliyotoka kutibuliwa na JKT Tanzania kwa kuchomolewa mabao dakika za jioni na kutoka sare ya 2-2 itakuwa na kazi mbele ya wageni waliotoka kushinda mabao 3-0 nyumbani dhidi ya Tabora. Hilo ni pambano la nne kwa timu hizo kukutana katika ligi tangu Namungo ilipopanda daraja msimu wa 2019-2020, lakin rekodi zikiibeba zaidi Mashujaa ambayo ni msimu wake wa pili kwani katika mechi hizo imeshinda mbili na sare moja.

Timu hizo zinakutana, huku mwenyeji kwenye mechi tano zilizopita akishinda mmoja, sare tatu na kupoteza mmoja wakati Mashujaa kwenye mechi tano imeshinda mbili, kufungwa mbili na sare mechi moja.

Makocha wa timu zote, Juma Mgunda wa Namungo na Salum Mayanga wa Mashujaa wametamba kwamba hautakuwa mchezo mwepesi, lakini muhimu ni kuzitumia dakika 90 kupata matokeo mazuri.