Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fei Toto atoa kauli nzito Azam FC

FEISAL Pict

Muktasari:

  • Azam ikiwa jijini Mbeya, jana ilifanya kweli kwa kuilaza Ken Gold mabao 2-0 na kubaki nafasi ya tatu na pointi 51, ikisaliwa na michezo sita kumaliza msimu.

KIUNGO wa Azam, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema mechi sita zilizobaki ni kucheza kufa na kupona kwani lolote linaweza kutokea katika vita ya ubingwa, huku akifichua siri kinachomkwamisha kufunga mabao.

Azam ikiwa jijini Mbeya, jana ilifanya kweli kwa kuilaza Ken Gold mabao 2-0 na kubaki nafasi ya tatu na pointi 51, ikisaliwa na michezo sita kumaliza msimu.

Hadi sasa Yanga ndio vinara wa ligi hiyo na pointi 61 baada ya michezo 23, huku Simba waliocheza mechi 22 wakifuata kwa pointi 57 na kufanya upinzani mkali kwenye ubingwa msimu huu.

Katika mechi sita zilizobaki za Azam, ni dhidi ya Singida BS (ugenini), Yanga (nyumbani), Kagera Sugar (ugenini), Dodoma Jiji (nyumbani), Tabora United na Fountain Gate ikicheza ugenini.

Kwa upande wa orodha ya wafungaji, Jean Ahoua (Simba) ndiye kinara wa mabao akitupia 12, huku Clement Mzize akiwa na 11 sawa na Prince Dube wote Yanga, huku Fei Toto akiwa na manne na asisti 12.

Alisema kinachowapa nguvu ni namna kila mchezaji anavyojituma na kufuata maelekezo ya kocha na kila mechi kwao ni vita ya pointi tatu kisha kusubiri hatma yao.

“Ushindani ni mkali kwenye ligi, lakini tunashukuru kila mmoja kikosini anapambana kadri ya uwezo wake, hatukati tamaa wala kubweteka badala yake tunatafuta pointi tatu kila mechi,” alisema nyota huyo.

Kuhusu ufungaji mabao, nyota huyo wa zamani wa Yanga alisema kutofunga kwa sasa ni kutokana na kutoa nafasi kwa wengine na timu haitegemei mtu mmoja.

“Ndiyo maana nikipata nafasi nikaona siko sehemu nzuri ya kufunga nampa aliye eneo zuri na timu inashinda na ndiyo lengo letu, najivunia kuwa kinara kwenye asisti za mabao,” alisema staa huyo wa kimataifa wa Taifa Stars.