Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fountain Gate yamkomalia Yusuphu Athuman

Muktasari:

  • Athuman amejiunga na timu hiyo akitokea Tanzania Prisons aliyokuwa anaitumikia kwa mkopo akitokea Fountain Gate ambao hakuwahi kuichezea mchezo hata mmoja.

SIKU chache baada ya mshambuliaji Yusuph Athuman kutambulishwa na Yangon United ya Ligi Kuu Myanmar, uongozi wa Fountain Gate imeibuka na kuweka wazi kuwa bado ni mchezaji wao halali.

Athuman amejiunga na timu hiyo akitokea Tanzania Prisons aliyokuwa anaitumikia kwa mkopo akitokea Fountain Gate ambao hakuwahi kuichezea mchezo hata mmoja.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Fountain Gate, Kidawawa Tabitha alisema Athuman bado ni mchezaji wao halali wamempeleka kwa mkopo wa miezi sita kwenye timu hiyo.

“Ni kweli ametambulishwa huko lakini haiondoi kuwa mchezaji wa Fountain Gate kwani sisi ndio tumempeleka huko kwa mkopo ili akaendeleze kipaji chake baada ya kushindwa kututumikia sisi kutokana na kipengele kigumu kilichokuwa kinatufunga kumtumia,” alisema na kuongeza:

“Hatukuweza kumtumia kwasababu tulishindwa kumuingiza kwenye mifumo ya usajili baada ya kufungiwa kusajili na ndio maana tulimtoa kwa mkopo kwenda Prisons kama bahjati kapata hiyo timu na kufikia makubaliano ya kumpekeka huko.”

Akizungumzia nafasi hiyo Athuman alisema ni nafasi nyingine kwake kupambania kipaji chake kwa kuisaidia timu yake hiyo mpya kufikia malengo waliyojiwekea msimu huu, kuhakikisha anajitoa kwa uwezo wake wote kuwa sehemu ya mafanikio ya timu hiyo.

“Najivunia kuwa sehemu ya timu ya Yangon United ni moja ya timu zenye mafanikio katika ligi ya Myanmar ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo nitajitoa kwa uwezo wangu wote kuhakikisha timu hii inatwaa ubingwa,” alisema.

Yangon United ipo nafasi ya pili ikikusanya pointi 51 kwenye mechi 22 walizocheza ikishinda 15, sare sita na kupoteza mchezo mmoja ipo nyuma kwa pointi 11 na kinara wa msimamo Shan United yenye pointi 62.