Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fountain yaziwekea mkakati pointi 6

Muktasari:

  • Fountain Gate ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi 28 ikifanikiwa kukusanya pointi 29, ina kibarua kigumu kuhakikisha inakwepa mtego wa kucheza playoffs katika mechi mbili zilizobaki.

KIKIOSI cha Fountain Gate chini ya kocha Khalid Adam, leo Jumapili kinarejea kwenye uwanja wa mazoezi kwaajili ya kujiweka tayari kwa dakika 180 zitakazoamua hatma yao.

Fountain Gate ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi 28 ikifanikiwa kukusanya pointi 29, ina kibarua kigumu kuhakikisha inakwepa mtego wa kucheza playoffs katika mechi mbili zilizobaki.

Akizungumza na Mwanaspoti, Adam ambaye anakaimu nafasi hiyo akichukua mikoba ya Robert Matano ambaye yupo nchini Kenya kujiuguza, alisema wana kibarua kigumu kupambania pointi sita kwenye mechi mbili zilizosalia.

“Hatuna sababu ya kuwaacha wachezaji waendelee kubaki majumbani mwao wakati timu haina matokeo mazuri na nafasi tuliyobaki nayo ni kupambania pointi sita zilizobaki kwa kupata matokeo ili tujiweke kwenye nafasi nzuri,” alisema na kuongeza:

“Wachezaji wote wanatakiwa kuripoti kambini jijini Arusha kwa ajili ya kujiweka tayari kwa mechi moja ya ugenini dhidi ya Coastal Union kisha tutamaliza na Azam FC kwenye uwanja wetu wa nyumbani, zote sio rahisi bila ya mipango thabiti.”

Adam alisema anaamini muda watakaokaa pamoja wakisawazisha makosa utaisaidia timu hiyo kukwepa kucheza mechi za mtoano (playoffs).

“Kazi kubwa niliyonayo sasa ni kupambana kuhakikisha napunguza makosa eneo la ulinzi kwani timu yangu ndio inaongoza kufungwa mabao mengi (54), hivyo ili niweze kuwa salama ni kutengeneza safu imara hasa kwenye hizi mechi mbili muhimu kwetu.”

Fountain Gate imefunga mabao 30 ikiruhusu 54, mawili zaidi ya yale ambayo imeruhusu KenGold (52), ambayo ilikuwa timu ya kwanza kushuka daraja msimu huu, kabla ya Kagera Sugar kuifuata huko Championship zitakakoshiriki msimu ujao wa 2025-26.