Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKU yaitupa nje Singida Black Stars Muungano Cup

Muktasari:

  • Katika muda wa dakika tisini, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2, huku Singida Black Stars ikiwa ya kwanza kufunga kupitia Victorien Adebayor dakika ya 6 na Iddi Khalid 'Gego' dakika ya 25.

JKU kutoka kisiwani Unguja, imefuzu nusu fainali ya Kombe la Muungano baada ya kuifunga Singida Black Stars ya Tanzania Bara kwa penalti 6-5 katika mchezo wa robo fainali ya kwanza uliochezwa leo Aprili 24, 2025 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.

Katika muda wa dakika tisini, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2, huku Singida Black Stars ikiwa ya kwanza kufunga kupitia Victorien Adebayor dakika ya 6 na Iddi Khalid 'Gego' dakika ya 25.

Tariq Mohamed alianza kuisawazishia JKU dakika ya 28 kwa mkwaju wa penalti kisha Fredy Seleman akafunga lingine dakika ya 45+3 na kufanya kwenda mapumziko matokeo yakiwa sare ya 2-2.

Kipindi cha pili hakikuwa na mabadiliko ya matokeo ndipo mikwaju ya penalti ikaamua mshindi.

Katika penalti nane zilizopigwa kila upande, Singida Black Stars ilikosa tatu kupitia Edward Charles Manyama, Joe Ephraim Makoye na Elvis Rupia, huku Damaro Mohamed Camara,

Frank Assinki, Victorien Adebayor, Anthony Tra Bi Tra na Edmund John wakifunga.

JKU penalti zao zilifungwa na Habeeb Abiola, Mohamed Ali, Tarik Mohamed Mikonga, James Ambrose, Hassan Makame na Mohamed Mtumwa, huku Abubakar Nidhar na Koffy Hamza wakikosa.

Mshindi wa robo fainali ya kesho Aprili 25, 2025 kati ya KMKM dhidi ya Azam itakayoanza saa 1:15 usiku kwenye Uwanja wa Gombani, atacheza nusu fainali na JKU, Aprili 28 mwaka huu uwanjani hapo.

Michuano hiyo inafanyika Uwanja wa Gombani ikishirikisha timu nane ambapo nne kutoka Bara na zingine Zanzibar. Itafikia tamati Mei Mosi mwaka huu.