Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Josiah, Ongala nani atatokelezea?

ONGALA Pict

Muktasari:

  • Endapo Prisons ikiifunga KMC yenye pointi 24 na ipo nafasi ya 11 itafikisha pointi 21 itapanda nafasi moja, jambo ambalo kocha Josiah analiona litawapa morali ya kuendelea kupambania timu, isishuke daraja.

POINTI 18 na nafasi ya 15 iliopo Tanzania Prisons, inamfanya kocha wa timu hiyo Amani Josiah kuwa na hesabu kali dhidi ya KMC kwani ikishinda mchezo wa Jumatano hii itapanda hadi nafasi ya 14 iliopo Kagera Sugar yenye alama 19.

Endapo Prisons ikiifunga KMC yenye pointi 24 na ipo nafasi ya 11 itafikisha pointi 21 itapanda nafasi moja, jambo ambalo kocha Josiah analiona litawapa morali ya kuendelea kupambania timu, isishuke daraja.

"Tunacheza na timu yenye uhitaji wa pointi kama sisi ingawa imetuzidi nafasi na ipo katika Uwanja wake wa KMC Complex, pamoja na hayo yote utakuwa mchezo mgumu na ushindani wa juu," alisema Josiah na kuongeza;

"Wachezaji wapo tayari na wenyewe hamu yao ni kuona tunaondoka nafasi ya chini, ndio maana tunauona ni mchezo unaohitaji hesabu kali kwa upande wetu."

Kama ilivyo kwa Josiah aliye na hesabu kali kwa mchezo huo, ndivyo ilivyo kwa kocha wa KMC, Kali Ongala anayeamini wakishinda watafikisha pointi 27 na timu hiyo itapanda hadi nafasi ya tisa itazishusha Mashujaa ilipo nafasi ya 10 ina pointi 24 na  Coastal Union nafasi ya tisa ina pointi  25. 

"Mechi za mwisho kwa ajili ya kufunga msimu ni ngumu, inahitaji hesabu na mbinu ya kushinda, tunacheza na Prisons inayojikwamua na kushuka daraja, hivyo natarajia ushindani utakuwa mkali," alisema.