Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kali Ongala siku 139 mechi tatu

ONGALA Pict

Muktasari:

  • Katika mechi hizo zote tatu alizoshinda, zimechezwa uwanja wao wa nyumbani wa KMC uliopo Mwenge, Dar es Salaam.

KOCHA Mkuu wa KMC, Kali Ongala amepata ushindi wake wa tatu ndani ya timu hiyo katika kipindi cha siku 139 tangu akabidhiwe kikosi hicho Novemba 14, 2024 akichukua nafasi ya Abdihamid Moallin aliyetimkia Yanga.

Katika mechi hizo zote tatu alizoshinda, zimechezwa uwanja wao wa nyumbani wa KMC uliopo Mwenge, Dar es Salaam.

Ushindi wa kwanza kwa kocha huyo ulikuwa Desemba 16, 2024 wa bao 1-0 dhidi ya Pamba Jiji kupitia bao la Hance Masoud dakika ya 88.

Baada ya hapo, akakaa kwa siku 56 Februari 10, 2025 aliposhinda tena mabao 2-0 dhidi ya Singida Black Stars mfungaji akiwa Oscar Paul dakika ya 35 na 40, kisha Aprili 2 akaichapa Tanzania Prisons 3-2 kwa mabao ya Shaban Idd Chilunda dakika ya 41 na 66, huku Ibrahim Elias akifunga dakika ya 55.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ongala alisema licha ya kuibuka na ushindi dhidi ya Tanzania Prisons, timu yake haikucheza vizuri kutokana na kushindwa kulinda vizuri nyavu zao zisitikiswe.

“Nimefurahi timu yangu imepata matokeo mazuri lakini bado nina kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha haya yanayotokea sasa hayajirudii kwenye mechi zilizo mbele yetu, nitakaa na wachezaji wangu kupanga mipango sahihi ya kumaliza mechi sita zilizobaki,” alisema na kuongeza.

“Timu ili iweze kupata matokeo mazuri inatakiwa kujengwa kuanzia eneo la ulinzi kwani washambuliaji wanaweza wakatumia nafasi walizotengeneza lakini wakaangushwa na safu ya ulinzi, ndicho kilichotokea, lakini huu sio wakati wa kulaumiana nitahakikisha timu inabadilika kila eneo na kuwa na ushindani hasa kwenye mechi zilizobaki ambazo zina umuhimu kwetu ili kujitengenezea mazingira mazuri mwisho wa msimu.”

Kocha huyo tangu akabidhiwe kikosi cha KMC, amekiongoza kwenye mechi 13, akishinda tatu zote nyumbani na kupoteza sita nne zikiwa nyumbani, huku sare ni nne.

Kwa jumla, KMC msimu huu kwenye ligi imecheza mechi 24, ikishinda saba, sare sita na kupoteza 11 ikikusanya pointi 27.