Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kapo ya Aziz KI, Hamisa Mobeto yawania tuzo

Aziz Pict

Muktasari:

  • Wanandoa hao wanawania tuzo ya Africa Golden Awards katika kipengele cha kapo bora ya mwaka tuzo zitakazotolewa, Aprili 5 mwaka huu huko Kenya.

SIKU chache baada ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI kufunga ndoa na mwanamitindo, Hamisa Mobetto kapo yao imewekwa kuwania tuzo.

Wanandoa hao wanawania tuzo ya Africa Golden Awards katika kipengele cha kapo bora ya mwaka tuzo zitakazotolewa, Aprili 5 mwaka huu huko Kenya.

Aziz KI na Hamisa wamechaguliwa kuwania tuzo hiyo ambayo pia wanashindania mastaa kibao kutoka Afrika.

Mastaa hao watachuana na mastaa wengine wa Tanzania, akiwemo muigizaji Zaylissa & Haji Manara, Vanessa Mdee na Rotimi (Nigeria), Priscilla Ojo& Juma Jux.

Mastaa wengine ni Davido & Chioma (Nigeria) ambao walifunga ndoa mwaka jana, Amberay & Kennedy Rapudo (Kenya), Kateclinton & Vincent Mackay (Rwanda), The WA Jesus Family (Kenya) na The Mamideb and Cleave (Uganda).

Zari Hassan & Shakib Cham (Afrika Kusini, Uganda), The Mziza's (Kenya), Ruby & Mocmadu (Nigeria), Miss Michuki & Jordan Lee (Kenya), Vanessa & Brad (Kenya, Marekani), Diana Marua na Bahati wa Kenya na Mr & Mrs Phoenix (Zimbabwe).