Katwila aipa tahadhari Mtibwa Sugar

Muktasari:
- Mwalwisi aliyejiunga na kikosi hicho akitoka TMA FC ya jijini Arusha aliyoiongoza katika michezo 15 ya raundi ya kwanza, alisema sare hiyo nyumbani imeharibu mipango yao, hivyo kilichobakia ni miujiza kutoka kwa wapinzani wao waliokuwa juu.
KOCHA wa Mbeya Kwanza, Maka Mwalwisi amesema kwa sasa timu hiyo ni ngumu kumaliza nafasi nne za juu kwa michezo miwili iliyobakia, baada ya kikosi hicho juzi kulazimishwa sare ya kufungana kwa mabao 2-2, nyumbani dhidi ya African Sports.
Mwalwisi aliyejiunga na kikosi hicho akitoka TMA FC ya jijini Arusha aliyoiongoza katika michezo 15 ya raundi ya kwanza, alisema sare hiyo nyumbani imeharibu mipango yao, hivyo kilichobakia ni miujiza kutoka kwa wapinzani wao waliokuwa juu.
“Malengo yetu yalikuwa ni kumaliza nafasi nne za juu ili tucheza michezo ya mtoano ‘Play-Off’, kwa hali ilivyo kwa sasa ni ngumu kutimiza hilo labda itokee miujiza kwa mechi mbili zilizobakia ila kiuhalisia mazingira sio rafiki,” alisema.
Kocha huyo aliyejiunga na kikosi hicho akichukua nafasi ya Emmanuel Masawe, ili amalize nafasi nne za juu ni lazima pia ashinde michezo miwili iliyobakia, huku akiiombea tena Geita Gold iliyopo nafasi ya nne na pointi zake 54, ipoteze yote.
Kiujumla Mbeya Kwanza imecheza michezo 28, ambapo kati ya hiyo imeshinda 14, sare saba na kupoteza pia saba, ikishika nafasi ya tano na pointi zake 49, huku eneo la ushambuliaji likifunga mabao 40 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 26.