Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Katwila asimulia mazito Championship

KATWILA Pict

Muktasari:

  • Geita Gold ambayo iliwahi kushiriki Ligi Kuu kabla ya kushuka daraja misimu miwili nyuma, imekuwa na matokeo mazuri ikiongoza msimamo kwa pointi 68 ambapo imebakiza mechi tatu kuhitimisha ligi hiyo.

WAKATI Geita Gold ikisaka pointi tatu pekee kurejea tena Ligi Kuu, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Zuberi Katwila amesema hataisahau Championship ya msimu huu, huku akifichua siri kwa timu hiyo.

Geita Gold ambayo iliwahi kushiriki Ligi Kuu kabla ya kushuka daraja misimu miwili nyuma, imekuwa na matokeo mazuri ikiongoza msimamo kwa pointi 68 ambapo imebakiza mechi tatu kuhitimisha ligi hiyo.

KATWI 01

Katika michezo mitatu iliyobaki hadi sasa, timu hiyo inahitaji pointi tatu tu kujihakikishia kuungana tena na Yanga na Simba, ambapo mchezo ujao itakuwa nyumbani mjini Geita kuikaribisha Songea United, Juni 7 katika uwanja wa Nyankumbu.

Iko hivi, iwapo timu hiyo itashinda mchezo huo itafikisha pointi 71, au ikipata pointi moja, itafikisha 69 ambapo Polisi Tanzania iliyopo nafasi ya tatu kwa pointi 60 ikishinda mechi tatu zote itaishia pointi 69 huku ikiwalazimisha Maafande hao ifunge zaidi ya mabao 17.

Katwila aliyewahi kuzinoa timu kadhaa za Ligi Kuu kwa mafanikio, anakumbukwa kwa rekodi ya kupandisha Ihefu Ligi Kuu (kwa sasa Singida Black Stars) na sasa anasaka historia nyingine kwa Geita Gold.

KATWI 02

Akizungumza na Mwanaspoti, Katwila amesema licha ya mafanikio hayo lakini hataisahau Championship ya msimu huu kutokana na upinzani walioupata na changamoto binafsi katika majukumu.

Amesema kwa muda mrefu amekuwa mkimya kwani ligi hiyo imejaa mambo mengi na ukiamua kufunguka unaweza kujikuta ukitofautiana na watu, huku akiwapongeza nyota wake, benchi la ufundi, uongozi na mashabiki kwa ushirikiano na sapoti kubwa ndani na nje ya uwanja.

“Tunahitaji ushindi katika mchezo ujao dhidi ya Songea United tuone tunatanguliza mguu Ligi Kuu, kiujumla ligi ni ngumu na ndio maana kwa muda mrefu nimekuwa kimya nifanye kazi ili initangaze yenyewe”

KATWI 03

“Niwashukuru wachezaji wamekuwa wakifuata kile ninachowaelekeza, lakini mashabiki na uongozi kwa ujumla wamekuwa sehemu ya mafanikio hadi sasa tunaposubiri dakika 90 za hatma yetu” amesema Katwila.

Kocha huyo amesema kuwa licha ya pointi tatu au moja wanayosubiri kwa sasa, lakini hesabu zake ni kusaka heshima nyingine ya ubingwa wa jumla wa ligi hiyo akieleza kuwa lazima historia iandikwe upya.