Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ng'ondya aanza tambo Geita Gold

NGODYA Pict

Muktasari:

  • Geita iliyoshuka daraja msimu wa 2023-2024, msimu huu ndio vinara wa Ligi ya Championship ikiwa na pointi zake 68, baada ya kushinda mechi 21, ikitoka sare tano na kupoteza moja kati ya 27, huku ikifunga mabao 60 na kuruhusu 15.

KIUNGO mshambuliaji wa Geita Gold, Richardson Ng'ondya amesema licha ya ushindani mkubwa wa wapinzani wao hadi sasa, ila timu hiyo ina nafasi ya kurejea Ligi Kuu, kutokana na ushirikiano wa wachezaji, mashabiki, viongozi na benchi la ufundi.

Nyota huyo amesema ubora wa benchi la ufundi na wachezaji wa kikosi hicho unawapa motisha ya kupambania malengo ya timu hiyo ili irejee Ligi Kuu, baada ya kushuka msimu wa 2023-2024, licha ya kasi na ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani.

"Licha ya kubaki mechi chache ila sisi wachezaji tunataka kumaliza vizuri kwa maana ya kubeba ubingwa wa Championship, ushindani wa wapinzani wetu ni chachu ya kupambana kwa lengo la kuhakikisha tunatimiza malengo yetu," amesema Ng'ondya.

Nyota huyo aliyecheza Azam FC chini ya miaka 20, African Sports, Ihefu ambayo kwa sasa ni Singida Black Stars na Mbeya City, amejiunga na Geita Gold msimu huu, baada ya kuachana na Kagera Sugar, huku akiwa tayari ameshaifungia mabao saba.

Geita iliyoshuka daraja msimu wa 2023-2024, msimu huu ndio vinara wa Ligi ya Championship ikiwa na pointi zake 68, baada ya kushinda mechi 21, ikitoka sare tano na kupoteza moja kati ya 27, huku ikifunga mabao 60 na kuruhusu 15.