Prime
Nyuma ya mastaa Yanga kuna hawa
KATIKA misimu minne mfululizo ya Yanga kutawala soka la Tanzania kwa kuchukua mataji ya Ligi Kuu Bara, mashabiki wa timu hiyo wamekuwa chachu ya mafanikio ya mastaa kwa nyakati tofauti.
Mashabiki wa timu hiyo wanashindwa kuficha hisia zao kwa wachezaji wao wanaofanya vizuri kwa kuwapa zawadi za fedha pamoja na kulitaja jina la mchezaji huyo kila kona jambo lililotajwa kuwa moja ya sababu ya mabingwa hao kufanya vizuri Ligi Kuu.
Kwa sasa mashabiki wa Yanga hauwambii kitu kwa kiungo mshambuliaji Allan Okello aliyejiunga na klabu hiyo msimu huu akitokea Vipers ya Uganda ndiye jina linatajwa zaidi na mashabiki wa klabu hiyo, kutokana na kiwango anachokionyesha hivi karibuni.
Okello mwenye miaka 25, katika mwezi huu pekee ameweka rekodi ya kufunga mabao tisa kati ya bao yake 11, asisti saba, akishika nafasi ya kwa ufungaji nyuma kinara kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliye na mabao 14, asisti nane.
Kabla ya Okello jina la Pacome Zouzoua ambaye amefunga mabao saba, asisti nne, 2024/25 lilikuwa na muendelezo wa kutajwa zaidi kutokana na alichokifanya 2024/25 ambapo alifunga mabao 12, asisti 10 alikuwa nguzo Yanga baada ya kuondoka kwa Stephane Aziz Ki.
Ingawa mshambuliaji Prince Dube kuna kipindi kiwango chake kinakuwa juu lakini mashabiki hao walilazimia kumfanyia maombi na kumtia moyo tayari msimu huu kaimbwa sana na amehusika katika mabao 13 kafunga mabao tisa na asisti nne.
Mbali na hao kuna muda nyota ya mshambuliaji Laurindo Dilson Depu iliwaka kabla ya kupata majeraha na kurejea tena na amefunga mabao sita.
Ukiachana na Depu, pia msimu wa 2023/24 Aziz Ki alikuwa na mabao 21 alikuwa namba mbili kwa kutoa asisti nyingi (nane) nyuma ya aliyekuwa winga wa Azam Kipre Junior aliyemaliza na tisa, lakini kwa mabao aliyemaliza nyuma ya Ki alikuwa Feisal Salum ‘Fei Toto’ alikuwa na mabao 19.
Jina la Aziz Ki lilikuwa juu baada ya kuondoka kwa Fiston Kalala Mayele ambaye kwa sasa anacheza Pyramids, umaarufu wa staa huyo ulitokana na kiwango chake ambapo msimu wa 2022/23 alikuwa kinara wa mabao 17 yalikuwa sawa na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Saido Ntibazonkiza.
Nyuma yake (msimu wa 2021/2022) Mayele alimaliza mfungaji wa pili kwa mabao 16 nyuma ya aliyekuwa mshambuliaji wa Geita Gold, George Mpole alikuwa na mabao 17.
Baada ya Aziz Ki kwenda kujiunga na Wydad msimu wa 2025/26 na sasa yupo Al-Ittihad Tripoli na anahusishwa kurejea Yanga ndipo alipoibuka Pacome.