Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amani Josiah, Minziro kazi zinazungumza

AMANI Pict

Muktasari:

  • Kuongea sana katika vyombo vya habari na kujisifia hakutoshi kumfanya mtu atoshe kuwa mchezaji au kocha mkubwa kwani mwishowe watu watahitaji kuona nini amekifanya ndani ya uwanja maana soka ni mchezo unaochezwa hadharani.

UZURI wa mchezo wa soka, kazi inayofanyika uwanjani ndio inatambulisha uwezo wa mtu kama ni mdogo, wastani au mkubwa hasa kwa makocha na wachezaji.

Kuongea sana katika vyombo vya habari na kujisifia hakutoshi kumfanya mtu atoshe kuwa mchezaji au kocha mkubwa kwani mwishowe watu watahitaji kuona nini amekifanya ndani ya uwanja maana soka ni mchezo unaochezwa hadharani.

Katika msimu ambao miezi mingi ya mwanzo haikuonekana kuwaendea vizuri makocha wazawa, wameibuka makocha wawili katika dakika hizi za lala salama ambao wameiacha kazi yao iongee sana kuliko midomo yao.

Wameonyesha vitu ambavyo angalau vinatupa furaha hapa kijiweni na kutupa imani angalau tunao makocha wazawa ambao wanaweza kufanya vitu spesho katika ligi yetu dhidi ya makocha wa kigeni.

Kuna kocha anaitwa Amani Josiah wa Dodoma Jiji. Kaifanya timu yake kuwa sumbufu kwa vigogo wa soka nchini ambao ni timu za Yanga na Simba.

Timu hizo mbili zimetolewa sana jasho na Josiah katika mechi walizokutana na Dodoma Jiji hivi karibuni. Mechi mbili za Ligi Kuu ambazo Dodoma Jiji ilikuwa nyumbani msimu huu dhidi ya Simba na Yanga, imechukua pointi, ikishinda moja na kutoka sare moja.

Halafu kuna kocha Felix Minziro. Alikabidhiwa Fountain Gate ikiwa hoi taabani lakini ndani ya muda mfupi ameibadilisha kuifanya iwe vizuri na sasa haipo katika kundi la timu zilizo katika hatari ya kushuka daraja.

Kijiwe hakina deni kwa Minziro na Amani Josiah kwa kile walichokifanya kwenye Ligi Kuu msimu huu japo wapo katika timu za kawaida. Wanastahili sifa na hapa hawawezi kuzikosa.