Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa kuikimbia JKT, Fountain kukutana na rungu

FOUNTAIN Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa kanuni ya 33 kifungu cha sita kinaeleza kuwa timu yeyote itakayogomea kuendelea na mechi itapigwa faini ya kiasi hicho na ushindi utapewa timu pinzani.

BAADA ya Fountain Gate Princess kugomea kuendelea na mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake juzi dhidi ya JKT Queens, itakumbana na adhabu ya kutozwa faini ya Sh 2 Milioni na kupokonywa ushindi.

Kwa mujibu wa kanuni ya 33 kifungu cha sita kinaeleza kuwa timu yeyote itakayogomea kuendelea na mechi itapigwa faini ya kiasi hicho na ushindi utapewa timu pinzani.

"Endapo timu itagomea kuendelea na mchezo kwa sababu zozote zile na kusababisha mchezo huo kuvunjika au kuvunjwa na mwamuzi timu hiyo itapoteza mchezo huo na timu pinzani itapewa ushindi. Timu iliyogomea itatozwa faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000/-)," inasema kanuni hiyo

"Faini iliyotajwa (kanuni 33:6) italipwa kabla ya mchezo unaofuata wa timu husika baada ya kuamriwa kulipa,"

"Mchezaji na kiongozi watakaobainika kugomea au kusababisha vurugu zilizopelekea mchezo kuvunjika watafungiwa kujihusisha na masuala yote ya mpira wa miguu kwa kipindi kati ya miezi sita mpaka miaka mitano."

Mchezo huo ulipgwa Uwanja wa KMC Complex na JKT ikiwa mwenyeji hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, walikuwa mbele kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na Anastazia Katunzi, Jamila Rajabu na Stumai Abdalah.

Sababu za kutoendelea kwa mchezo huo ni kitendo cha Fountain Gate Princess kutorudi uwanjani kipindi cha pili, huku ikidaiwa timu hiyo haikuridhishwa na uamuzi wa waamuzi katika baadhi ya matukio.

Kocha wa JKT Queens, Ester Chaburuma, ameliambia Mwanaspoti kuwa, hawafahamu nini kiliwakuta wapinzani wao kwani wao waliporudi uwanjani kwa ajili ya kuendelea na kipindi cha pili, wenzao hawakutokea.

"Hatujui nini kiliwakuta (Fountain Gate Princess) kwa sababu walicheza vizuri sana kipindi cha kwanza na hakukuwa na vurugu za kusema kuwavamia waamuzi wala nini.

"Baada ya kurudi kipindi cha pili, waamuzi wamefanya kama ilivyotakiwa kukaa muda husika na timu pinzani haikutokea, wakaondoka msimamo wetu sisi tumemaliza mechi na tunajipanga na mchezo wa mwisho wa ligi," amesema Chaburuma.

Hata hivyo tulipowatafuta viongozi wa Fountain hawakupatikana lakini tulimpata Kaimu Kocha Mkuu, Noah Kanyanga aliyesema kwa ufupi "Ni jambo la utawala siwezi kuzungumza watafute wao ndio," alisema Kanyanga

Tulipomdodosa kwamba ilikuwaje wameondoka uwanjani ilikuwa mipango au viongozi waliwaambia waondoke akajibu "Nimeshakwambia siwezi kuongeza liko nje ya uwezo wangu."