Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisinda ampa wakati mgumu Waziri JR Iraq

WAZIRI Pict

Muktasari:

  • Msuva ambaye amefunga mabao 12 kwenye ligi hiyo maarufu 'Iraq Stars League' amekuwa akipata nafasi ya kuanza kwenye kikosi hicho mara kwa mara wakati Wazir Jr anaanzia benchi kwenye kikosi chake.

WAKATI Simon Msuva akiendelea kukiwasha Ligi Kuu ya Iraq akiwa na Al Talaba, Mtanzania mwenzake, Wazir Jr Shentembo anayekipiga Al Mina'a mambo yanaonekana ni magumu tangu alipojiunga na chama hilo.

Msuva ambaye amefunga mabao 12 kwenye ligi hiyo maarufu 'Iraq Stars League' amekuwa akipata nafasi ya kuanza kwenye kikosi hicho mara kwa mara wakati Wazir Jr anaanzia benchi kwenye kikosi chake.

Wazir Jr ambaye aliwahi kukipiga Yanga msimu wa 2020/21, alijiunga na timu hiyo iliyopo nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi yenye timu 20, kwa mkataba wa miezi sita mwanzoni mwa msimu huu na tangu atambulishwe kikosini hapo Februari 05 mwaka huu, hajapata nafasi ya kuanza moja kwa moja kwenye timu hiyo.

Hata hivyo, Mkongomani, Tuisila Kisinda ambaye pia aliwahi kuwika na Yanga kwa misimu tofauti 2020/21 na 2022/23 akitokea AS Vita ya nchini kwao anaonekana ndiye anayemweka benchi Mtanzania huyo ambaye wanacheza nafasi moja na katika mechi nane za mwisho amefunga mabao mawili.

Mmoja wa watu wa karibu wa Wazir Jr, aliliambia Mwanaspoti kinachomweka benchi mshambuliaji huyo sio kiwango bali chaguo la kocha. "Kocha wa mwanzo ndiye aliyempendekeza Wazir kusajiliwa lakini tangu aondoke ni kama huyu mpya akubali uwezo wake," alisema mtu huyo.