Kissu awafunika Diarra, Manula

Muktasari:

  • Kissu aliyejiunga na kikosi hicho msimu huu baada ya kuachana na KMC, alifunga bao hilo kwa mpira wa  ‘goalkick’ alioupiga na ukaenda moja kwa moja wavuni baada ya kumpita kipa wa Polisi Tanzania aliyekuwa amevutika mbele na kuizamisha timu hito 2-0, katika mchezo mkali na wa kusisimua uliopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Mara.

Kipa wa Biashara United, David Kissu Mapigano ameweka rekodi msimu huu katika Ligi ya Championship baada ya kufunga bao, huku akiwapiku pia makipa wengine wakiwemo wa Ligi Kuu Bara kama Aishi Manula wa Simba na Djigui Diarra wa Yanga.


Kissu aliyejiunga na kikosi hicho msimu huu baada ya kuachana na KMC, alifunga bao hilo kwa mpira wa  ‘goalkick’ alioupiga na ukaenda moja kwa moja wavuni baada ya kumpita kipa wa Polisi Tanzania aliyekuwa amevutika mbele na kuizamisha timu hito 2-0, katika mchezo mkali na wa kusisimua uliopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Mara.


Akizungumzia bao hilo kipa huyo alisema, kwake sio mara ya kwanza kufanya hivyo kwa sababu anakumbuka msimu wa 2019/2020 akiichezea Gor Mahia ya nchini kwao Kenya alifunga pia wakati kikosi hicho kiliposhinda mabao 3-0, dhidi ya Bandari FC.
“Kwangu ni fahari. niliwahi kufunga katika mazingira na maeneo yaleyale kwa dakika zilezile,” alisema.
Kipa Juma Kaseja wakati akidakia Yanga ilifunga bao kama hilo dhidi ya Toto Africans wakishinda 2-1 na kuipa Yanga ubingwa 2008-09.