Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Azam aibua matumaini mapya

Muktasari:

  • Kiungo huyo aliumia mfupa mdogo wa kidole kidogo cha mguu na kufanyiwa upasuaji mdogo ikitazamiwa majeraha yake yatapona kuanzia wiki ya sita tangu kuanza kwa matibabu.

BAADA ya awali kuelezwa huenda kiungo wa Azam FC, Adolf Mtasingwa atakosa mechi zote za Ligi Kuu Bara zilizobaki, taarifa mpya ni kwamba anaweza kuziwahi zile za kumalizia msimu.

Kiungo huyo aliumia mfupa mdogo wa kidole kidogo cha mguu na kufanyiwa upasuaji mdogo ikitazamiwa majeraha yake yatapona kuanzia wiki ya sita tangu kuanza kwa matibabu.

Mara ya mwisho kiungo huyo mkabaji ambaye amekuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza kucheza ilikuwa Februari 15 mwaka huu dhidi ya Mashujaa ambapo Azam ilishinda 2-0 katika Ligi Kuu Bara.

Tangu aumie, kiungo huyo amekosekana kwenye mechi tano zikiwemo nne za Ligi Kuu Bara na moja Kombe la FA ambapo kati ya hizo Azam imeshinda moja, imepoteza moja na sare tatu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Daktari wa Azam FC, Mbarouk Mlinga, alisema Bitegeko ameshaacha kutembea kwa msaada wa magongo mawili na sasa anatumia moja.

Mlinga alisema wakati kiungo huyo akionyesha maendeleo hayo ameshaanzishiwa mazoezi tiba ili kuweka mwili wake sawa kwa kuwa aliumia sehemu ndogo ya mguu.

“Unajua aliumia kwenye kidole chake... tayari ameshaacha kutembea kwa msaada wa magongo mawili na sasa anatumia moja pekee, lakini kwa maendeleo yake tumeona pia aanze mazoezi ya tiba maungo ili kuweka mwili wake sawa.

“Kwa maendeleo yanavyoonekana tunaamini anaweza kuwahi baadhi ya mechi hizi za mwisho tofauti na tishio la awali ambalo tulidhani anaweza kukosa sehemu yote ya msimu iliyosalia.

“Tukiona anazidi kuimarika na kila kitu kitakuwa sawa tutawakabidhi makocha waendelee naye kwa matumizi yao,” alisema daktari huyo.

Katika hatua nyingine, daktari huyo amethibitisha kwamba kiungo mwingine mkabaji Sospeter Bajana, yuko sawa kuendelea na majukumu ya kikosi hicho hatua ambayo itawapa nguvu makocha wa kikosi hicho.

Bajana na Bitegeko wanacheza eneo moja la kiungo mkabaji ambapo kukosekana kwao anacheza Yahya Zayd, Ever Meza na James Akaminko.