Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha African Sports ala kiapo

AFRICAN Pict

Muktasari:

  • Hadi sasa timu hiyo imecheza michezo 24 msimu huu ya Ligi ya Championship ambapo kati yake imeshinda minne, sare miwili na kupoteza 18, ikishika nafasi ya 14 na pointi zake 14, huku eneo la ushambuliaji likifunga mabao 21 na kuruhusu 46.

LICHA ya African Sports ‘Wanakimanumanu’ kuandamwa na ukata, kocha wa timu hiyo, Kessy Abdallah amesema siyo sababu ya yeye kushindwa kukibakisha kikosi hicho katika Ligi ya Championship msimu ujao, huku akiomba wadau kuwasapoti zaidi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kessy alisema kwa wiki kadhaa sasa wamekuwa wakipitia hali hiyo ingawa jambo wanaloshukuru ni kwenda kwa wakati katika vituo vya mchezo husika hasa ile ya ugenini, tofauti na wangekuwa hawana uwezo huo wa kusafiri.

“Ni wakati mgumu lakini hilo sio tatizo sana kwa sababu tunasafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, nafikiri kwangu ni changamoto kubwa ila kama kocha lazima nionyeshe mfano kwa wachezaji kwa kuwapa motisha ya kupambana zaidi,” alisema.

Timu hiyo ambayo ni mabingwa wa Kombe la Muungano mwaka 1988, imepanda Ligi ya Championship msimu huu baada ya kushuka daraja msimu wa 2022-2023 iliposhika nafasi ya 14 na pointi 23, huku msimu uliopita ikiwa ndio mabingwa wa First League.

Hadi sasa timu hiyo imecheza michezo 24 msimu huu ya Ligi ya Championship ambapo kati yake imeshinda minne, sare miwili na kupoteza 18, ikishika nafasi ya 14 na pointi zake 14, huku eneo la ushambuliaji likifunga mabao 21 na kuruhusu 46.