Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Al Nassr ampa u-MVP Clara Luvanga

CLARA Pict

Muktasari:

  • Ligi ya Wanawake Saudia ilitamatika wikiendi iliyopita na Al Nassr ilinyakua ubingwa ukiwa wa tatu mfululizo kwa klabu hiyo anayokipiga Mtanzania pekee Clara.

KOCHA Mkuu wa Al Nassr ya wanawake, Aziz Alalwni amemtaja nyota wa kimataifa wa Tanzania, Clara Luvanga ndio mchezaji anayestahili tuzo ya mchezaji bora wa mwaka.

Ligi ya Wanawake Saudia ilitamatika wikiendi iliyopita na Al Nassr ilinyakua ubingwa ukiwa wa tatu mfululizo kwa klabu hiyo anayokipiga Mtanzania pekee Clara.

Kupitia maoni aliyotoa kwenye mtandao wa kijamii alisema nyota huyo wa timu ya taifa ‘Twiga Stars’ anastahili tuzo hiyo kutokana na juhudi kubwa alizozionyesha msimu huu.

Alalwni aliandika “Asante sana, wewe kweli ni bora, umetoa mchango mkubwa sana kwa timu hii na umekuwa sababu kuu ya mafanikio yote tuliyoyapata. Hakuna mshambuliaji kama wewe,” aliandika kocha huyo na kuongeza:

“Kipaji chako, juhudi zako, na kujitolea kwako vimekuwa vya kipekee kabisa, Msimu huu umekuwa wa kipekee kwa sababu yako. Bila shaka wewe ndiye Mchezaji Bora wa Msimu wetu (MVP), umeacha alama kubwa, na tunajivunia sana kuwa na wewe kwenye timu yetu.”

Huu ni msimu wa pili kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga Princess kuitumikia Al Nassr iliyobeba ubingwa bila kupoteza mchezo wowote kwenye mechi 16 za ligi hiyo ilizocheza.

Msimu huu Clara amefunga mabao 20 na asisti saba akivunja rekodi ya msimu uliopita aliyofunga mabao 11 na asisti saba.

Timu hiyo ilibeba ubingwa kabla ya msimu kumalizika ikiwa raundi ya 14 tu na jumla imekusanya pointi 48.