Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lwanga awapa somo viungo

New Content Item (1)
New Content Item (1)

TADDEO Lwanga ni moja kati ya viungo wakabaji bora wanaopatikana barani Afrika kwa siku za hivi karibuni na hilo amelithibitisha katika meche mbali mbali alizocheza akiwa na Simba pia timu ya Taifa ya Uganda 'The Cranes'.

Tangu ajiunge na Simba katika dirisha dogo la msimu huu lililofungwa Januari 15 Lwanga aliingia moja kwa moja kwenye kikosi cha wanamsimbazi hao na kuleta mabadiliko makubwa chanya ndani ya timu hiyo.

Mwanaspoti limepiga Stori na Lwanga kuhusu ubora wake ambapo ameweka wazi mbinu ambazo kiungo mkabaji anapaswa kuzitumia ili kuwa bora katika kutimiza majukumu yake.

"Nipo bora kwasababu najua majukumu yangu katika timu, ukiwa kiungo namba sita inabidi uwe na akili kubwa ya kusoma mchezo lile ndio eneo ambalo fujo na mambo mengine magumu hutendeka hivyo inabidi na wewe uendane nayo ili kupunguza presha ya wapinzani," amesema Lwanga.

Lwanga amekuwa na muendelezo mzuri wa kiwango chake na katika mchezo wa jana dhidi ya AS Vita Club, Simba ikishinda bao 4-1 alicheza dakika zote 90 huku akipiga jumla ya pasi 34 bila kupoteza hata moja.