Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mapya yaibuka bondia aliyezimia ulingoni Dar, ahamishiwa Moi

Muktasari:

  • Tatizo hilo liligundulika mchana wa jana Jumatatu Januari 27, 2024 baada ya kufanyiwa kipimo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke hali iliyolazimu kuandikiwa rufaa ya kupelekwa Muhimbili.

BONDIA wa Ngumi za Kulipwa Tanzania, Mohamedi Mnemwa, amepewa rufaa ya kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwenye kitengo cha Mifupa Moi kufuatia kipimo cha CT Scan kuonyesha damu imevilia kwenye ubongo.

Tatizo hilo liligundulika mchana wa jana Jumatatu Januari 27, 2024 baada ya kufanyiwa kipimo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke hali iliyolazimu kuandikiwa rufaa ya kupelekwa Muhimbili.

Januari 24, 2025, bondia huyo alizimia baada ya kupigwa Technical Knockout (TKO) raundi ya tatu katika pambano la raundi nne dhidi ya Ally Issa Sewe lililofanyika Ukumbi wa Mrina uliopo TipTop, Manzese jijini Dar es Salaam.

Daktari wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Dokta Hadija Hamisi, amesema: "Mgonjwa ameshafanyiwa kipimo cha CT Scan na amegundulika kuwa damu imevilia kwenye ubongo, anapelekwa Moi, Muhimbili kwa ajili ya kupata vipimo zaidi na Moi watatupa majibu zaidi."

Kwa taarifa zaidi kuhusu hali ya bondia huyo endelea kufuatilia mitandao yetu.