Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchezaji mpya wa Simba SC afunguka

Muktasari:

  • Usajili wa Athumani umetokana na kiwango bora alichoonyesha katika Ligi Kuu na Kombe la FA ambacho kilimvutia Aussems.

Dar es Salaam. Winga mpya wa Simba, Miraji Athumani amesema jukumu lake la kwanza ni kupambana kupata namba katika kikosi cha kwanza.

Athumani alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kutia saini mkataba wa kujiunga na Simba akitokea Lipuli ya Iringa.

Alisema kabla ya kufanya uamuzi wa kurejea Simba alijipima kama ana uwezo wa kucheza kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezaji huyo alisema anatambua Simba na ina wachezaji nyota katika safu ya ushambuliaji, lakini hawawezi kuwa kikwazo kwake kupata nafasi ya kuonyesha kipaji chake.

 “Mpaka nimeamua kusaini Simba nitakuwa nimemalizana na Lipuli lakini uzoefu na majina ya wachezaji wakubwa waliokuwa Simba haunipi hofu, nitapambana,” alisema Athumani.

Alisema hawezi kukata tamaa kwa kuwa kazi yake ni kucheza mpira na changamoto za namba aliwahi kukutana nazo alipojiunga na Toto African ya Mwanza kabla ya kutua Lipuli.

Alisema kitendo cha kujiunga na Simba ni ishara kuwa kocha Patrick Aussems ameridhika na kiwango chake uwanjani.

Mchezaji huyo alisema ameanza kufanya mazoezi binafasi ya ufukweli ili kujiandaa kwa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza Agosti, mwaka huu.

 “Jambo la msingi kila nikipata nafasi ya kucheza nitafanya kile ambacho benchi la ufundi watakuwa wamenipa maelekezo,” alisema winga huyo wa kulia.

Usajili wa Athumani umetokana na kiwango bora alichoonyesha katika Ligi Kuu na Kombe la FA ambacho kilimvutia Aussems.

 Winga huyo aliyetokea kikosi cha vijana cha Simba, anakwenda kuziba nafasi ya Shiza Kichuya.

Aussems alisema usajili wa Athumani umefanyika kulingana na mahitaji ya ripoti yake aliyoacha kwa viongozi wa Simba.