Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Minziro: Hatuhitaji kuchoma sindano kucheza mechi ngumu

Minziro Pict

Muktasari:

  • Huo utakuwa mchezo wa pili kwa timu hizo kukutana msimu huu katika ligi kwani mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Azam Complex, jijini Dar es Salaam Yanga waliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0.

KOCHA Mkuu wa Pamba Jiji, Fred Felix 'Minziro' amesema kutokana na upana wa kikosi chake na ubora wa kila mchezaji baada ya usajili wa dirisha dogo hawahitaji kuwachoma sindano baadhi ya wachezaji kuwalazimisha wacheze hata pale wanapokuwa na uchovu ama majeraha.

Miinziro ametoa kauli hiyo akizungumzia maandalizi ya timu ya Pamba kabla ya kukabiliana na Yanga jioni ya leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Amesema kutokana na mfululizo wa mechi za Ligi Kuu unasababisha majeraha ya mara kwa mara na uchovu kwa wachezaji, jambo ambalo hata hivyo halimpi wasiwasi mkubwa anapokwenda kuikabili timu ngumu ya Yanga hapo kesho kwani anajiamini upana wa kikosi chake unampa ujasiri.

"Fatiki imekuwa kubwa uchovu unapokuwa mkubwa lazima kila mchezaji umpe nafasi ya kucheza. Tuna kikosi kipana hilo linatisaidia hatuna haja ya kudunga sindano mchezaji kwamba lazima acheze hapana, tunashukuru kila nafasi tuna wachezaji walau wawili hadi watatu hiyo inatusaidia," amesema Minziro.

Minziro aliyetua Pamba Oktoba 17, 2024 na kuiongoza katika mechi 15 za Ligi Kuu, amesema mchezo wa leo Ijumaa ni mgumu na mashabiki wategemee mchezo mzuri kwani wanahitaji kuvuna ushindi ili wajinasue kutoka nafasi za chini.

"Watu wategemee kuona mechi nzuri hatuendi pale tu kupoteza mchezo tuko nafasi za chini kwahiyo kuna ushindani mkubwa wa aina yake lazima tujipapatue kutoka chini," amesema Minziro na kuongeza;

"Kwa ujumla watu wategemee kuona mechi nzuri sana tunakutana na timu ambayo ni bora ina wachezaji wazuri unapokuatana na timu bora lazima uwe na mbinu mbadala ambazo zitakufanya uendane na mchezo."

Kiungo wa Pamba Jiji, Paulini Kisindi amesema timu hiyo ina kikosi chenye ubora wa kucheza dhidi ya Yanga na wachezaji wenye uzoefu na wapya wana hamu ya kucheza mchezo huo na kuonyesha ubora wao kwamba Pamba haijasajili wachezaji waoga.

"Ni faida sana kuwa na wachezaji ambao wana uzoefu na mechi hizi kwenye timu ni mechi ambayo tunakwenda kufurahia na hata wachezaji wapya wanatamani kesho waonyeshe nchi nzima kwamba Pamba haijasajili wachezaji waoga," amesema Kisindi na kuongeza;

"Mashabiki wa Pamba kwenye nyakati zote ngumu wamekuwa na sisi kesho tunawaahidi utakuwa mchezo mzuri na kuvuna alama tatu kama alivyofanya Tabora na timu zingine na mwisho wa siku wafurahi na kushangilia."