Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NYEPESI NYEPESI ZA DABI: Simba mvua, Yanga Jumamosi

MVUA Pict

Muktasari:

  • Enzi hizo siku ya kupigwa dabi iwe ni Jumapili kisha mvua inyeshe kabla ya mchezo huo, Simba ilikuwa ikiimini inashinda na haikushangaza matokeo yakawa upande wao mara kadhaa.

SIJUI ni maendeleo au kitu gani, lakini unaambiwa miaka kadhaa ya nyuma kulikuwa na imani flani zilizokuwa zikiwafanya mashabiki wa Simba na Yanga kubashiri matokeo ya mechi za Dabi ya Kariakoo za ligi kabla hata hazijachezwa.

Enzi hizo siku ya kupigwa dabi iwe ni Jumapili kisha mvua inyeshe kabla ya mchezo huo, Simba ilikuwa ikiimini inashinda na haikushangaza matokeo yakawa upande wao mara kadhaa.

Kwa upande wa Yanga yenyewe iliamini jua likiwaka na mchezo huo ukipigwa Jumamosi, basi walikuwa wakitembea kifua mbele mapema kwa kuamini wanashinda na matokeo huwa upande wao.

Pia hata zile kambi zilizokuwa zikiwekwa na klabu hizo kabla mchezo, Yanga ikipenda Bagamoyo au Pemba na Simba Unguja, kwa sasa hazipo kuonyesha kuwa dabi imebadilika.