Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pedro aichorea Simba ramani ya Dabi

RAMANi Pict


YANGA imethibitisha akili yao ipo kwenye Kombe la Muungano, pia kuna hesabu zinapigwa kwa siri kufikiria mechi ngumu dhidi ya Simba itakayopigwa Mei 3, mwaka huu ikisema hilo haliepukiki.


Yanga imetinga nusu fainali ya Kombe la Muungano ikionyesha inataka kutetea taji la ubingwa huo ikienda kukutana na Azam, wakati Simba ilikuwa inacheza mchezo wake wa kwanza jana usiku dhidi ya Mafunzo.


Endapo Yanga itafanikiwa kutinga fainali kwa kuiondoa Azam, huku Simba ikishinda dhidi ya Mafunzo na kukutana na mshindi kati ya Mlangege na Singida Black Stars nako ikashinda, basi timu hizo zitakutana kwenye fainali ya Kombe la Muungano, Aprili 29, 2026.

RAMA 06
RAMA 06

Wakati ratiba ikinukia kuwa hivyo, mapema tu Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, ameliambia Mwanaspoti kuwa licha ya kwamba hawataki kuchanganya mambo, akili zao hivi sasa zimejikita kwenye mechi za Muungano, lakini Simba wanaiangalia kwa mbali.

RAMA 03

Pedro amesema kwasasa wataendelea kuweka mkazo kwenye mechi za Muungano ambapo wanataka kutetea ubingwa wao, lakini bado kuna mambo mengine ya kujipanga yataendelea taratibu.

“Hatutaki kuchanganya mambo sana, kwasasa akili yetu kubwa itakuwa kwenye mechi za Muungano, sisi ni mabingwa watetezi na bado tunataka kuyalinda mafanikio yetu ya msimu uliopita,” amesema Pedro.

“Siwezi kukataa kwamba hatufikirii mchezo dhidi ya Simba, kuna nafasi lazima muangalie namna ya kupanga mambo yenu ya mbele, kuna maeneo juu ya maisha ya wachezaji na matumizi yao, lazima yazingatie ugumu wa mechi hiyo.”

RAMA 04

Pedro aliongeza kuwa, hata Simba inapita njia hiyo hiyo ikitambua kwamba hautakuwa mchezo rahisi kwa timu zote lakini timu yake haina presha na mchezo huo.

“Kitakachoendelea kwetu nafahamu pia itakuwa hivyo kwa Simba, ukweli ni kwamba hautakuwa mchezo rahisi kwa timu zote lakini niseme kwetu sisi Yanga hatuna presha na mchezo huo wakati ukifika tutajiandaa sawasawa.

“Nafahamu haitakuwa mechi sawa na ile ambayo tulikutana kwenye mzunguko wa kwanza, presha itaongezeka kwa kuwa kila timu inataka kuongeza uwezekano wa kuchukua ubingwa,” amesema Pedro.

RAMA 02

Msimu huu, Yanga na Simba tayari zimekutana mara mbili, ikianza Ngao ya Jamii ambapo Yanga ilishinda kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mechi nyingine ni ya duru la kwanza katika Ligi Kuu Bara, iliyopigwa Machi Mosi 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar ambapo ilimalizika bila ya kufunga.

Ushindani wa Yanga inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara msimu huu dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi tano, unazidi kuufanya mchezo ujao wa Dabi ya Kariakoo kuteka hisia za wengi huku kila upande ukichukua tahadhari.