Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ratiba Ligi Kuu Zanzibar yapanguliwa

GOFU Pict

Muktasari:

  • Katika mzunguko wa 29, ni michezo miwili tu ndiyo imefanyiwa mabadiliko ya tarehe ya kuchezwa ambayo itafanyika Juni 6 ni Uhamiaji na New Stone Town kwenye Uwanja Mao A na Muembe Makumbi City dhidi ya Fufuni kwenye Dimba la Mao B.

KAMATI ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya Ligi Kuu Zanzibar, imefanya mabadiliko madogo ya ratiba ya ligi hiyo kwa sababu ya kupisha Sikukuu ya Eid El Hajj.

Mabadili hayo yamefanywa kwa mzunguko wa 27, 28 na 29 ambapo tarehe zake zimebadilishwa, hivyo Mei 31, kutachezwa michezo mitatu.

Junguni United itaikaribisha Mlandege kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba, wakati Uwanja wa Mao A kisiwani Unguja, Kipanga itacheza dhidi ya Mafunzo huku Mao B hapohapo Unguja, New King itapambana dhidi ya Zimamoto.

Juni Mosi kutapingwa michezo mitatu, Chipukizi United dhidi ya Polisi kwenye Uwanja wa Gombani, KMKM itavaana na New Stone Town pale Mao B na JKU itaminyana na Fufuni kwenye Uwanja wa MAo A.

Mabadiliko hayo ni ya mechi za mzunguko wa 27. Kwa mzunguko wa 28, mechi tatu zitachezwa Juni 3, ambapo Uhamiaji itaikabili New King  kwenye Uwanja wa Mao B, Chipukizi United dhidi ya Mlandege kwenye Uwanja Gombani na Muembe Makumbi City itaonyeshana kazi na Mafunzo kwenye Dimba la Mao A.

Juni 4, KMKM dhidi ya Fufuni kwenye Dimba la Mao A, JKU na New Stone Town (Mao B) na Junguni United itacheza na Polisi katika Uwanja wa Gombani. Juni 5, Malindi itacheza na Kipanga kwenye Uwanja wa Mao B na KVZ watapepetuana na Zimamoto kwenye Uwanja wa Mao A.

Katika mzunguko wa 29, ni michezo miwili tu ndiyo imefanyiwa mabadiliko ya tarehe ya kuchezwa ambayo itafanyika Juni 6 ni Uhamiaji na New Stone Town kwenye Uwanja Mao A na Muembe Makumbi City dhidi ya Fufuni kwenye Dimba la Mao B.