Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni vita nusu fainali FA Pemba

FA ZNZ Pict

Muktasari:

  • Hatua hiyo ya nusu fainali kutakuwa na vita kubwa ikihusisha timu tatu za Ligi Daraja la Kwanza ambazo ni Wawi Star, Mwenge na Chakechake, huku moja pekee kutoka Ligi Kuu Zanzibar ambayo ni Chipukizi United.

NUSU fainali ya kwanza ya Kombe la FA Ukanda wa Unguja, inatarajia kupingwa Mei 24, mwaka huu kwenye Uwanja wa Gombani kati ya Wawi Star dhidi ya Chakechake.

Hatua hiyo ya nusu fainali kutakuwa na vita kubwa ikihusisha timu tatu za Ligi Daraja la Kwanza ambazo ni Wawi Star, Mwenge na Chakechake, huku moja pekee kutoka Ligi Kuu Zanzibar ambayo ni Chipukizi United.

Ikumbukwe bingwa mtetezi wa kanda ya Pamba ni Chipukizi United ambayo ilipoteza fainali ya kusaka bingwa wa jumla Zanzibar katika michuano hiyo dhidi ya KMKM.

Unaweza kusema Chipukizi United ni wababe wa FA Cup Ukanda wa Pemba kwani imelichukua mara nyingi kuliko timu yoyote kisiwani hapo, pia ndiyo inayoongoza kucheza fainali nyingi za FA Cup.

Timu itakayofanikiwa kuingia fainali, itasubri mshindi kati ya Chipukizi United dhidi ya Wembe na nusu fainali ya pili itachezwa Mei 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Gombani.