Samatta mambo magumu Ugiriki

Muktasari:
- Msimu wake wa kwanza akiwa PAOK 2023/24 Samatta alicheza mechi 29 za mashindano yote akifunga mabao mawili huku msimu huu akicheza mechi sita akiwa hana bao.
NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Samatta mambo yanaonekana kuwa magumu kwa upande wake akiwa na PAOK ya Ugiriki amekuwa akikosa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu yake hiyo.
Msimu wake wa kwanza akiwa PAOK 2023/24 Samatta alicheza mechi 29 za mashindano yote akifunga mabao mawili huku msimu huu akicheza mechi sita akiwa hana bao.
Tangu msimu 2024/25 uanze mambo yamekuwa magumu kwa Samatta ambaye anaonekana hayupo kwenye mipango ya kocha Rzvan Lucescu, raia wa Romania ambaye amekuwa akimuweka benchini mara kadhaa.
Juzi mshambuliaji huyo wa zamani wa Aston Villa ya Ligi Kuu England, hakuwa sehemu ya kikosi kilichosafiri kwenda Hispania kwenye mchezo wa Europa League dhidi ya Real Sociedad iliyopata ushindi wa mabao 2-0.
Msimu huu Samatta hajafunga wala kutoa asisti kwenye mechi sita za mashindano yote aliyocheza akitumika kwa dakika 257, huku Fedor Chalov akicheza zaidi yake.