Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Selemani Bwenzi ageuka lulu sokoni

BWENZI Pict

Muktasari:

  • Kikosi hicho kimeshuka daraja na msimu ujao kitashiriki Ligi ya Championship kutokana na kutokuwa na mwenendo mzuri hadi sasa, kikiburuza mkiani na pointi zake 16, baada ya kushinda mechi tatu, sare saba na kupoteza 17 kati ya 27 iliyocheza.

VIGOGO mbalimbali nchini wameanza kupiga hesabu za kuinasa saini ya mshambuliaji wa KenGold, Selemani Bwenzi kutokana na kiwango bora anachoonyesha akiitumikia timu hiyo, licha ya kikosi hicho kushuka daraja kikisaliwa na mechi tatu za ligi mkononi.

Kikosi hicho kimeshuka daraja na msimu ujao kitashiriki Ligi ya Championship kutokana na kutokuwa na mwenendo mzuri hadi sasa, kikiburuza mkiani na pointi zake 16, baada ya kushinda mechi tatu, sare saba na kupoteza 17 kati ya 27 iliyocheza.

Licha ya hayo, Bwenzi amekuwa kivutio kwa timu mbalimbali zinazowinda saini yake, ambapo Mwanaspoti linatambua wazi mojawapo ni Mtibwa Sugar iliyopanda Ligi Kuu na Geita Gold ambazo zote zimeonyesha uhitaji wa nyota huyo kwa msimu ujao.

Taarifa za ndani ambazo Mwanaspoti imezipata zinaeleza Mtibwa imeanza kumpigia hesabu nyota huyo kimyakimya, huku Geita ikikabiliwa na changamoto ya kuinasa saini yake, ikiwa itashindwa kurejea Ligi Kuu Bara msimu ujao kwa mechi za mtoano.

"Mtibwa imeonyesha nia lakini mchezaji mwenyewe hajafanya uamuzi kwa sababu ofa ni nyingi na msimu bado haujaisha, kwa sasa anahitaji kucheza Ligi Kuu, hivyo Geita isipopanda ni ngumu kumpata," alisema mmoja wa watu wa karibu na mchezaji huyo.

Kwa upande wa Bwenzi alipotafutwa na Mwanaspoti kuhusu hatima yake, alisema kwa sasa ni mapema kuzungumzia hilo, ingawa mashabiki wake watafahamu muda mwafaka ukifika, kama ataendelea kusalia KenGold au ataamua kutafuta changamoto kwingine.

"Kwanza nichukue nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki zetu kwa kile kilichotokea, tulipambana ili kuinusuru timu ila kwa bahati mbaya imeshuka, kuhusu hatima yangu kikosini naomba tumalize msimu kisha tutazungumzia hayo baadaye," alisema.

Kabla ya kujiunga na KenGold, nyota huyo alikuwa Mbeya Kwanza inayoshiriki Ligi ya Championship aliyoifungia bao moja na kuasisti mengine mawili, ambapo ameonyesha kiwango bora na kikosi hicho licha ya kushuka daraja na kurejea kilikotoka.

Bwenzi aliyesajiliwa Januari 2025, anashika nafasi ya pili kwa nyota wa kikosi hicho waliochangia mabao mengi ya timu hiyo, baada ya kufunga matano na kuasisti moja, akizidiwa na Mishamo Michael aliyefunga pia matano na kuasisti mawili.