Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys, Uganda ni kisasi

Muktasari:

Wakati timu ya Taifa ya U-17 (Serengeti Boys) imekamia kulipa kisasi dhidi ya Uganda katika fainali za Chalenji, serikali na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wanafanya kikao leo kujadili ushiriki wa Tanzania katika mashindano mbalimbali ya fainali za Afrika.

Dar es Salaam. Wakati timu ya Taifa ya U-17 (Serengeti Boys) imekamia kulipa kisasi dhidi ya Uganda katika fainali za Chalenji, serikali na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wanafanya kikao leo kujadili ushiriki wa Tanzania katika mashindano mbalimbali ya fainali za Afrika.

Serengeti Boys itachuka dimbani kwenye Uwanja wa Rubavu katika mechi ya kisasi kutokana na rekodi ya Uganda.

Katika fainali za 2018, Serengeti Boys ilifungwa bao 3-1 na Uganda kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.

Mwaka jana, Tanzania ilikubali kipigo cha bao 1-0 katika mechi ya hatua ya makundi ya Afcon, ambayo Tanzania ilikuwa mwenyeji.

Kutokana na rekodi hiyo, Kocha wa Serengeti Boys, Maalim Saleh ‘Romario’ alisema mechi ya leo ni ya kufa au kupona kwani wanataka kuweka rekodi mpya kwa kushinda dhidi ya Uganda.

“Tunajua haitakuwa mechi rahisi kutokana na Uganda kuwa timu ngumu, lakini tumejiandaa kushinda na kuongeza heshima zaidi pamoja na kufanikiwa kufuzu fainali za Afcon nchini Morocco, mwakani,” alisema Saleh.

Alisema kuwa vijana wake wamejiandaa vyema na wapo tayari kwa ‘vita’ dhidi ya Uganda.

Kocha wa Uganda, Hamza Lutalo pia ana malengo ya kulitetea vyema taji hilo kwa kushinda dhidi ya Tanzania.

Lutalo alisema wanataka kurejea rekodi ya 2018 pamoja na kutabiri mgumu wa mchezo huo.

Wakati huo huo; Serikali na TFF zinakutana leo kujadili maandalizi ya timu tatu za Tanzania ambazo zimefuzu fainali za mashindano ya Afrika na moja ya wanawake ambayo inawania nafasi ya kufuzu kombe la dunia.