Simba Queens V JKT Queens kupigwa Mei 07

Muktasari:
- Maboresho hayo ya ratiba ya Ligi Kuu Wanawake yametolewa hivi karibuni na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kufuatia mrundikano wa ratiba ya mashindano ya CAF.
DABI ya wanawake kati ya Simba Queens na JKT Queens imesogezwa mbele kutoka April 29 hadi Mei 07 kupisha mashindano ya timu ya taifa ya Futsal.
Maboresho hayo ya ratiba ya Ligi Kuu Wanawake yametolewa hivi karibuni na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kufuatia mrundikano wa ratiba ya mashindano ya CAF.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) yanafanyika Morocco kuanzia Aprili 22 hadi 30.
Ikumbukwe timu ya taifa Tanzania imepangwa kundi C na Madagascar, Senegal huku kundi B likiwa na Angola, Misri na Guinea ilhali A likiongozwa na waandaaji wa mashindano hayo Morocco, Cameroon na Namibia.
Kwenye kikosi cha timu ya taifa, baadhi ya nyota muhimu wameitwa JKT ikitoa nyota saba na Simba watano.
Hivyo sasa mchezo huo utapigwa Mei 07 kwenye Uwanja wa Mej Gen Isamuhyo ambapo JKT itakuwa nyumbani kuikaribisha Simba.
Mchezo uliopita zilipokutana timu hizo Simba ikiwa nyumbani iliambulia sare ya 1-1 Uwanja wa KMC Mwenge.
Mechi nyingine zilizosogezwa mbele ni Bunda v Fountain Gate Princess itakayopigwa Mei 2, Fountain v Mashujaa na Bunda na Alliance Girls Mei 06.