Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yarudi kivingine kusaka straika

SIMBA Pict


SIMBA bado haijakata tamaa kutafuta saini ya mshambuliaji Souleymane Fofana, lakini kama ikitokea amekosekana, basi ina chaguo lao la pili.


Simba inaendelea kupigania saini ya staa na mfungaji bora pale ASEC Mimosas ambaye ni Fofana anayeongoza kwa ufungaji akifunga mabao 14 kwenye ligi ya Ivory Coast, lakini ikitokea ikashindwa basi kuna Kevin Bakare.


Bakare ndiye mshambuliaji mwenye namba nzuri kando ya Fofana na Simba imepata jina lake na sasa inapambana naye ikimweka tayari katika uwezekano wa kumsajili wakati wa dirisha kubwa la usajili.

SIMB 02

Rekodi zinaonyesha, msimu huu Bakare ameshafunga mabao manane akiwa ndiye mfungaji bora namba mbili katika timu hiyo huku akitoa asisti tatu.

Simba inahitaji kusajili mshambuliaji mmoja au wawili kwa dirisha lijalo la usajili, ikilenga kuongeza nguvu eneo hilo ambalo msimu huu mpaka sasa linabebwa na mzawa Seleman Mwalimu aliyefunga mabao sita kwenye ligi.

Taarifa za ndani ya Wekundu hao wa Msimbazi zimeliambia Mwanaspoti, endapo Simba itampata Bakare, basi itakuwa ni kama imemsajili mshambuliaji wao wa zamani, Meddie Kagere kutokana na ubora wake.

SIMB 01

“Ukimwangalia huyu Sangare ni kama Meddie (Kagere) mwingine, anajua sana kufunga, kuna mtu wetu anayejua vipaji anamfuatilia kwa makini wakati tunatafuta kujua hatma ya huyu Fofana, tunaona kama ofa ni nyingi lakini hatujakata tamaa tunapambana.

“Ikitokea tukamkosa Fofana huyu Bakare atakuwa ni chaguo letu la pili, kama tukipata viungo wazuri ambao tunataka kuwatafuta basi tutakuwa tumeongeza mtu sahihi kabisa kwenye eneo la ushambuliaji yetu,” kilisema chanzo.

Ili kukamilisha dili hilo, Simba bado itatakiwa kumalizana na ASEC ili kumpata Bakare ambaye alijiunga na klabu hiyo Julai 2025 akiwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu ndani ya mabingwa hao wa kihistoria nchini Ivory Coast.