Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri saba za kurudisha ufalme Jangwani

YANGA Pict


YANGA inapiga hesabu namna ya kuyatetea mataji yake mawili yaliyosalia na hapo hapo imeanza kufanya upembuzi wa kikosi chake kwa hesabu za msimu ujao ambapo kuna uwezekano mkubwa ikasajili mastaa saba wapya wenye ubora, ikianza kuunda kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.


Mabosi wa timu hiyo wamekaa na kocha wao wa muda Abdihamid Moalin na kukubaliana ili kurudisha ubora wa kikosi chao kwa msimu ujao watalazimika kufanya usajiliwa wa wachezaji wapya wasiopungua saba ambao watakuwa na ubora wa kuja kuiongezea nguvu kwenye timu hiyo ambayo msimu huu iliondolewa kwenye hatua ya makundi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Ikumbukwe Yanga msimu huu ilisajili wachezaji 14 kupitia madirisha mawili ya usajili ambao iliamini wataiimarisha timu hiyo lakini ni wanne pekee ambao waliweza kupata nafasi katika mechi za timu hiyo ambayo inataka kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la CRDB ikiwa kileleni kwa sasa.

YANG 02

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema mabosi wa klabu hiyo wako kwenye msako wa kutafuta beki mmoja wa kati mzawa, viungo wawili wakabaji ambalo ndio litakuwa na msisitizo kutokana na kukosekana kwa mtu sahihi aliyeweza kufanya kazi kama ilivyofanywa na Khalid Aucho ambaye aliachana na klabu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika.

“Tunataka  kutafuta beki mmoja wa kati akiwa mzawa itakuwa safi, ili aje kusaidiana na Bacca (Ibrahim Abdullah), Job (Dickson), tunaamini atakuwa amepona sawasawa na Bakari (Mwamnyeto) kama tukipata mtu bora zaidi mzawa tutamuachia  Frank Asisinki ili nafasi yake tutafute mchezaji mwingine.

Hapo kwa mabeki wa kati bado tunaangalia sana tunaweza hata kumtoa mmoja kati ya hawa watatu waliokuwepo sasa wa ndani, tunataka kupaimarisha sana hapo, eneo lingine litakuwa kiungo mkabaji.

YANG 01

“Tunataka kusajili wawili, tuwe wakweli katika wote tuliowaleta hakuna ambaye ameweza kutusahaulisha kazi aliyofanya Aucho, kuna kitu tunakikosa ambacho tulikuwa tunakipata, sasa tutaweka mkazo, tukipata mmoja wa kigeni mzuri na mmoja mzawa itakuwa safi.”

Aidha ripoti hiyo pia inataka kusajiliwa kwa viungo washambuliaji wawili ambao ni namba kumi na mawinga lakini pia washambuliaji wawili mmoja akiwa mzawa na mwingine wa kigeni.

“Tunatafuta pia namba kumi mzuri atakayeweza kuja kusaidiana na Allan Okello, tumneona ameanza kuonyesha kilicho bora, kifupi huyu ndiye Okello ambaye tulikuwa tunamtaka lakini itakuwa safi tukipata mwingine wasaidiane unajua timu nzuri ni ile inayokuwa na watu wawili bora halafu wanashindana kupata nafasi.

YANG 04

“Tunataka pia kusajili winga mmoja, tukipata anayetumia mguu wa kushoto itakuwa safi au tukipata wa kulia itakuwa pia safi lakini muhimu awe na kasi na uwezo wa kufungua ukuta wa wapinzani.

“Tumepata tabu sana eneo hili la winga kwa msimu wa tatu sasa, kuna yule Ikangalombo (Jonathan) alishindwa kukidhi kiwango tukamrudisha, amekuja Buba Jamel bado hatujaona kile ambacho tuliambiwa na kocha wetu anacho.

“Tunataka pia washambuliaji wawili mmoja wa kigeni, lakini tukipata mzawa anayejua kufunga itakuwa nzuri hapa nako tutaweka nguvu kubwa, unajua washambuliaji wazuri wana gharama lakini Yanga inahitaji watu bora ili kufanya vizuri.

YANG 03

Wachezaji ambao Yanga iliwasajili msimu huu ni pamoja na kipa Hussein Masalanga, mabeki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Frank Assinki,Abubakar Nizar ‘Ninju’, viungo Lassine Kouma, Celestin Ecua, Mamadou Doumbia, Offen Chikola,Abdulnasir Abdallah ‘Casemiro’, Mohammed Damaro,Buba Jammeh,Mousa Bala Conte, washambuliaji wakiwa Emmanuel Mwanengo na Laurindo Aurelio ‘Depu’.

Katika wachezaji hao ni nane pekee waliosalia kwenye kikosi hicho wakimalizia msimu huu ambao ni Masalanga, Casemiro, Ninju, Damaro, Buba, Kouma, Mwanengo na Depu huku wengine Conte, Chikola, Doumbia na Ecua wakitolewa kwa mkopo kwenye klabu tofauti ambapo kuna baadhi wanacheza na wengine wapo benchi.

Wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu ambao wamekuwa wakionekana kwenye mechi za timu hiyo ni pamoja na Tshabalala, Okello, Damaro na Assinki, huku wengine wakiendelea kusotea benchi wakikosa ushawishi wa kupangua nafasi kweye kikosi hicho.

Kwa sasa Yanga ipo kileleni kwenye ligi ikiwa na pointi 60 mbili mbele ya Simba yenye pointi 58 zikiwa zimebaki mechi mbili tu ili msimu umalizike.