Tamil, Titans watoa visago kriketi ya T20

Muktasari:

  • Wakicheza katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  Tamil Nadu  waliweza kuwabamiza Dar Tigers kwa wiketi 5 katika mchezo wa kricket wa ova 20 uliochezwa siku yakatika  sikukuu ya Eid, June 17 mwaka huu.

ILIKUWA ni  sikukuu ya Eid  njema kwa timu za Tamil Nadu na Patel Titans baada ya timu hizo kuwapa wapenzi wake zawadi njema ya ushindi mnono.

Wakicheza katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  Tamil Nadu  waliweza kuwabamiza Dar Tigers kwa wiketi 5 katika mchezo wa kricket wa ova 20 uliochezwa siku yakatika  sikukuu ya Eid, June 17 mwaka huu.

Katika mchezo  huo, Dar Tigers ndiyo walioshinda kura na wakachugua kuanza kubeti na kufanikiwa kutengezeza mikimbio 129 huku wakiangusha wiketi 9.

Kwa ujasiri, Tamil Nadu waliweza kuzifikia alama  hizo kwa kupata mikimbio 132 huku wakiangusha wiketi 5 na hivyo kushinbda kwa wiketi 5.

Licha kufungwa, mchezaji Junaid Raza  wa Dar Tigers aling’ara kwa kutengeneza  mikimbio 46 kati ya 129 ambayo timu yake ilitengeneza     

Katika mchezo mwingine wa ova 20 uliofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Patel Titans  waliwaadhibu Caravans D kwa mikimbio 56 katika mchezo ulielemea upande mmoja.

Caravans D ndiyo walioshinda kura ya kuanza na kuamua kuzuia kwanza na kazi hiyo iliweza kuwapatia Patel Titans jumla ya mikimbio 99 huku wakiangisha wiketi tisa.

Kazi ya kuyafukuzia matokeo hayo ilionekana ngumu sana kwa  Vijana Caravands D kwani jitihada zao zote ziliishia kwenye mikimbio 41 baada ya wapiga fimbo wake wote 10 kutolewa na hivyo kuwafanya Patel Titans kuondoka na ushindi mnono wa mikimbio 56.

Hafidh Amiri alikuwa ndiye nyota wa mchezo wakati Colly Ambogo aliyetengeneza mikimbio  21 ndiye aling’ara kwa upigaji. .

Katika hatua nyingine,  Ligi ya kriketi kwa vijana wasiozidi miaka 17 itaendelea katika viwanja mbalimbali jijini siku ya Jumamosi hii.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na chama cha mchezo wa kriketi nchini (TCA), Kinondoni Boys itawakaribisha Annadil Burhan katika viwanja vya Leaders  wakati  uwanja wa Dar es Salaam Gymkhana utakuwa ni shahidi wa  mechi kati ya KSIJ Boys Red na KSIJ Boys Green.

Siku hiyo hiyo katika viwanja vya Leaders Kinondoni, Chanika Boys wataumana na vjana wa Indian School.

Uwanja wa Dar es Salaam  Gymkhana utamalizia siku kwa mechi kati ya Ilala Boys na Future Force Academy.